Tazama magoli yote matano na penati aliyokosa Alikiba katika mchezo wa hisani, Team FEIBUI ikiitandika Team SAMAKIBA mabao 3-2 kwenye Dimba la Amaan Complex, Zanzibar. Magoli ya FEIBUI (Fesal Salum Feitoto na Abdulaziz Makame) yamefungwa na Feisal Salum, Ibrahim Ahmada Hilika, na Dismas Novatus huku magoli ya SAMAKIBA (Mbwana Samatta na Alikiba) yakifungwa na Kelvin John 'Mbappe' na Mbwana Samatta. Dakika ya 24, Team SAMAKIBA walipata penati lakini Alikiba alikosa....
NIFUATE 2023: Team Samatta chini ya mwanandinga Mbwana Samatta imeendeleza ubabe dhidi ya Team Kiba iliyo chini ya msanii Alikiba kwa kupata ushindi wa mabao 4-2 katika mchezo wa hisani chini ya #SamakibaFoundation uliopigwa leo kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Abdul Suleiman Sopu amepiga #hattrick dakika ya 45', 63' na 71 huku goli lingine likifungwa na John Bocco aliyefungua mlango wa magoli dakika ya 21. Magoli ya Team Kiba yametoka kwa Ayoub Lyanga 69 na Msanii wa bongo fleva, Mario dakika ya 90'+4. Haya hapa magoli... #Nifuate2023 #NifuateDay #SamakibaFoundation #SAMAKIBA #TeamSamatta #TeamKiba #UpendoWaZambarau #SamattaFriends #AlikibaFriends #UpendoWaZambarau
SAMAKIBA 2022: Team Kiba iliyo chini ya msanii Alikiba imebeba Kombe la Nifuate 2022 kwa kuichapa Team Samatta iliyo chini ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia sare ya mabao 3-3. Katika muda wa kawaida, magoli ya Team Kiba yamefungwa na Saimon Msuva aliyefunga mawili pamoja na Alikiba mwenyewe kwa penati huku magoli ya Team Samatta ayakifungwa na Kelvin John, Mbwana Samatta na Idd Gamba kwa penati. Mechi hii ni tamasha maalum la hisani kwa ajili ya kurejesha jamii ambalo hufanyika kila mwaka chini ya taasisi ya Samakiba Foundation, na mwaka huu limefanyika kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, na kushuhudia Team Kiba wakibeba ndoo.