Mbeya City ilivyolazimishwa sare (1-1) dhidi ya Geita Gold
Mbeya City ilivyolazimishwa sare (1-1) dhidi ya Geita Gold

Haya ni magoli mawili yaliyopataikana katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa VPL kati ya Geita Gold FC dhidi ya Mbaya City uliopigwa leo Julai 29, 2020 mkoani Geita na kushuhudia timu hizo zikienda sare ya goli moja kwa moja. #GeitaGoldFC #GeitaGold #MbeyaCity #Mbeya #Geita #VPLPlayoffs #VPL #VodacomPremierLeague #LigiKuuTanzaniaBara Tazama taarifa ya Habari na vipindi vingine vya Habari na Matukio LIVE kutoka Azam TV na UTV kupitia Azam TV Decoder au AzamTV Max App. Unaweza kupata AzamTV Max App kwa ajili ya Android kutoka hapa: ► https://bit.ly/2wB6zmR Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz

Ihefu ilivyoanza vyema kampeni ya kupanda ligi kuu VPL kwa kuichapa (2-0) Mbao FC
Ihefu ilivyoanza vyema kampeni ya kupanda ligi kuu VPL kwa kuichapa (2-0) Mbao FC

Tazama magoli yote yaliyopatikana katika mchezo wa mkondo wa kwanza mtoano kati ya Ihefu dhidi ya Mbao FC uliochezwa katika dimba la Highland Estates, Mbarali mkoani Mbeya. #IhefuFC #VPLPlayoffs #TPL #MbaoFC #IhefuMbao Tazama taarifa ya Habari na vipindi vingine vya Habari na Matukio LIVE kutoka Azam TV na UTV kupitia Azam TV Decoder au AzamTV Max App. Unaweza kupata AzamTV Max App kwa ajili ya Android kutoka hapa: ► https://bit.ly/2wB6zmR Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz

MWADUI FC 2-1 GEITA GOLD FC; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (8/6/2019)
MWADUI FC 2-1 GEITA GOLD FC; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (8/6/2019)

Timu ya Mwadui FC imefanikiwa kusalia Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Geita Gold FC magoli 2-1 kwenye mchezo wa mtoano (playoff) uliopigwa kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga Mwadui ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mfungaji bora wa klabu hiyo Salim Aiyee dakika 33 kabla ya Baraka Jerome kusawazisha dakika 50. Wakati jahazi la Mwadui likielekea kuzama, dakika ya 90 Salim Aiyee akaiokomboa timu yake kwa kuaindikia goli la pili goli ambalo lilimaliza ndoto ya Geita kucheza ligi kuu

MAGOLI YOTE: MWADUI FC 2-1 GEITA GOLD FC; (PLAYOFF - 08/06/2019)

TFF yafafanua Kagera Sugar na African Lyon kushuka daraja
TFF yafafanua Kagera Sugar na African Lyon kushuka daraja

Ni rasmi timu za African Lyon ya Dar es Salaam na Kagera Sugar ya Kagera zimeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na msimu ujao zitacheza Ligi Daraja la Kwanza. Mwadui FC na Stand United za Shinyanga zitacheza mechi za mtoano dhidi ya timu za Geita Gold FC na Pamba SC kuamua kubaki au kuondoka kwenye ligi kuu. African Lyon imemaliza ligi ikiwa mkiani na pointi 23 huku Kagera Sugar ikiwa na pointi 44, sawa na Stand United na Mwadui wakitofautiana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku matokeo baina ya Kagera Sugar na Stand mara mbili walizokutana (Head-to-Head) pia yakichangia anguko hilo la Kagera Sugar Mwadui itacheza mtoano na Geita Gold ya Daraja la Kwanza huku Stand ikitarajiwa kucheza na Pamba kuwania kubaki ligi kuu, wakati wapinzani wao wakiwaniA kupanda daraja.

MTIBWA SUGAR 1-2 KCCA: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (CAF CC - 22/12/2018)
MTIBWA SUGAR 1-2 KCCA: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (CAF CC - 22/12/2018)

Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, imetupwa nje ya michuano wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya leo kuchapwa 2-1 na KCCA ya Uganda katika mchezo wa maruadiano uliopigwa kwenye Dimba la Chamazi Dar es Salaam. Kwenye mchezo huo, KCCA ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 28 kupitia kwa Muzamiru Mutyaba kabla ya Salum Kihimbwa kusawazisha dakika ya 51, na kisha wageni hao kutoka Jijini Kampala Uganda kupata bao la pili dakika ya 87 kupitia kwa Allan Okello. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jijini Kampala nchini Uganda, KCCA ilipata ushindi wa mabao 3-0, na hivyo inafuzu kuingia hatua ya mtoano kwa jumla ya magoli 5-1, huku Mtibwa ambayo hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki michuano ya CAF tangu mwaka 2002, ikifungashiwa virago.

Utetezi wa Simba baada ya kuchapwa 1-0 na Mbao FC, Mwanza (TPL - 20/09/2018)
Utetezi wa Simba baada ya kuchapwa 1-0 na Mbao FC, Mwanza (TPL - 20/09/2018)

Meneja wa timu ya Simba Abbas Ally amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutulia na kujiandaa na furaha katika mechi zijazo baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili mfululizo. Abbas ametoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Mbao FC uliomalizika kwa Simba kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Septemba 20, 2018. Amesema ligi siyo mashindano ya mtoano bali ina mechi mechi nyingi hivyo atakayemaliza vizuri ndiye atakaye kuwa bingwa, na Simba bado ina nafasi hiyo. Kuhusu mabadiliko ya Kocha wa timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji, Abbas amesema kocha anapanga kikosi kulingana na jinsi wachezaji walivyofanya mazoezi na mchezaji atakayeonekana kuwa vizuri zaidi ndiye anayepewa nafasi kwenye mechi. Kwa upande wake beki wa Simba ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amewataka mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa baada ya kufungwa na Mbao FC.

« Previous

Popular Tags

#Zlatan Ibrahimovi  #Kobe Bryant  #Best Ball Controls  #Michael Jordan  #Sergio Aguero  #Golden State Warriors  #Cristiano Ronaldo  #Los Angeles Lakers  #Football Defensive Skills  #Neymar  

Popular Users

#rihanna  #instagram  #TimTebow  #mcuban  #realDonaldTrump  #JJWatt  #BizNasty2point0  #geniebouchard  #tigerwoods  #sydneyleroux  #ATLHawks  #J_No24  #WWE  #oldhossradbourn  #MichelleDBeadle