TFF yafafanua Kagera Sugar na African Lyon kushuka daraja by @Azam TV - Post Details

TFF yafafanua Kagera Sugar na African Lyon kushuka daraja

Ni rasmi timu za African Lyon ya Dar es Salaam na Kagera Sugar ya Kagera zimeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na msimu ujao zitacheza Ligi Daraja la Kwanza. Mwadui FC na Stand United za Shinyanga zitacheza mechi za mtoano dhidi ya timu za Geita Gold FC na Pamba SC kuamua kubaki au kuondoka kwenye ligi kuu. African Lyon imemaliza ligi ikiwa mkiani na pointi 23 huku Kagera Sugar ikiwa na pointi 44, sawa na Stand United na Mwadui wakitofautiana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku matokeo baina ya Kagera Sugar na Stand mara mbili walizokutana (Head-to-Head) pia yakichangia anguko hilo la Kagera Sugar Mwadui itacheza mtoano na Geita Gold ya Daraja la Kwanza huku Stand ikitarajiwa kucheza na Pamba kuwania kubaki ligi kuu, wakati wapinzani wao wakiwaniA kupanda daraja.

Similar Posts!

Yanga SC 2-1 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 20/04/2024
Yanga SC 2-1 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 20/04/2024

KARIAKOO DERBY: Yanga SC imeendeleza ubabe kwa kuichapa Simba mabao 2-1 kwa mara ya pili msimu huu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC #NBCPremierLeague uliopigwa leo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Magoli ya Yanga yamefungwa kipindi cha kwanza na Stephane Aziz Ki kwa penati dakika ya 20 na Joseph Guede dakika ya 38.

USIKU WA VITASA | Karim Mandoga Vs Mada Maugo (TKO) - 11/04/2024
USIKU WA VITASA | Karim Mandoga Vs Mada Maugo (TKO) - 11/04/2024

Kwa TKO raundi ya sita, Mada Maugo amemkalisha Karim Mandonga.

Mashujaa FC 1-1 (6-5) Simba SC | Penati | CRDB Bank Federation Cup - 09/04/2024
Mashujaa FC 1-1 (6-5) Simba SC | Penati | CRDB Bank Federation Cup - 09/04/2024

Tazama mikwaju yote ya penati iliyopigwa kwenye mchezo CRDB Bank Federation Cup kati ya Mashujaa FC dhidi ya Simba SC. Simba imetolewa kwa jumla ya penati 6-5 Waliopiga kwa upande wa Simba ni Mohamed Hussein, Israel Mwenda, Freddy Michael Koublan, Willy Onana, Mzamiru Yassin, Ladack Chasambi, Sadio Kanoute Waliopiga kwa upande wa Mashujaa ni Zuberi Dabi, Samson Madeleke, Masinda, Idrissa Stambuli, Adam Adam, Mpoki Mwakinyuke, Baraka Mtui

Yanga kupeleka malalamiko CAF yaliyojiri mechi yao na Mamelodi Sundowns
Yanga kupeleka malalamiko CAF yaliyojiri mechi yao na Mamelodi Sundowns

“Kama klabu lazima tuoneshe kwamba kuna namna ambavyo hatujaridhishwa na kile ambacho kimetokea katika mchezo ule” sehemu ya maneno ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe akizungumzia hatua ambazo timu hiyo imepanga kuzichukua juu ya yale yaliyojiri katika dimba la Loftus kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

MSHIKESMSHIKE VIWANJANI - 03/04/2024
MSHIKESMSHIKE VIWANJANI - 03/04/2024

Tazama taarifa mbalimbali za maandalizi ya Simba na Yanga SC kuelekea mechi zao za marudiano za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika.

MSHIKEMSHIKE VIWANJANI 01/04/2024
MSHIKEMSHIKE VIWANJANI 01/04/2024

Tazama kipindi cha Mshikemshike Viwanjani ambacho kimekusanya habari mbalimbali ikiwemo taarifa ya Rais wa Yanga, Hersi Said akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo. Mashabiki wa Yanga wameanza safari ya kwenda Mamelodi

Azam FC 2 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 17/03/2024
Azam FC 2 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 17/03/2024

DAR DERBY: Yanga SC imeangukia pua kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC, katika #DarDerby iliyopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Yanga imetangulia kupata bao kupitia kwa Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Azam kuchomoa dakika ya 19 kwa goli la Gibril Sillah na kisha Feisal Salum akafunga la ushindi dakika ya 51.

Magoli | Azam FC 2-1 Yanga SC | NBC Premier League 17/03/2024