Content removal request!


MAGOLI: AZAM FC 2-1 RUVU SHOOTING (TPL - 22/11/2018)

Azam FC imepata ushindi wa mabao 2-1 ikiwa kwenye Dimba lake la nyumbani Azam Complex Chamazi Dar es Salaam dhidi ya Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi. Mabao ya Azam kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ dakika ya 11 ya mchezo na Tafadzwa Kutinyu dakika ya 66 huku bao pekee la Ruvu Shooting likifungwa na Said Dilunga dakika ya 27. Matokeo haya yanaifanya Azam FC kufikisha pointi 33 kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imecheza jumla ya mechi 13 huku ikiendelea kulinda rekodi yake ya kutopoteza mchezo wowote hadi sasa tangu kuanza kwa ligi msimu huu.