Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga SC umemalizika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Kwa sare hiyo, Yanga SC inajisogeza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutokana na kujiongezea pointi moja na kufikisha 13 baada ya kucheza mechi tano, nne nyingine zote wakishinda. Kwa upande wao, mabingwa watetezi, Simba SC wanafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi sita, wakitoa sare ya pili leo na kufungwa moja, nyingine tatu wakishinda. Lakini Simba SC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na pointi zote kwenye mchezo wa leo, kwani walifanikiwa kuwazidi wapinzani wao muda wote Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars