AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 05/03/2019)
AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 05/03/2019)

African Lyon wameendelea kupoteza matumaini ya kusalia ligi kuu Tanzania Bara baada ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania, katika mchezo uliopigwa kwenye Dimba l Uhuru Dar es Salaam. Wageni JKT ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kupitia kwa Hassan Mwaterema kabla ya Hood Mayanja aliyeingia dakika ya 72, kuisawazishia Lyon dakika ya 75. Kwa matokeo hayo JKT Tanzania imepanda kutoka nafasi ya tisa hadi ya sita ikiwa na pointi 36 sawa na Mbao FC pamoja na Alliance FC huku African Lyon ikiendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22.

MAGOLI: AFRICAN LYON 1-1 JKT TANZANIA (TPL - 05/03/2019)

Msimamo, Simba ni Hatari Fire African Lyon Waibariki Simba
Msimamo, Simba ni Hatari Fire African Lyon Waibariki Simba

Klabu Ya Simba ni Hatari Fire African Lyon Waibariki Simba. Msimamo wa Ligi Kuu baada ya Mechi za Leo Klabu ya Simba yasogea hadi nafasi ya Tatu. #AfricanLyonVsSimba #SimbaVsAfricanLyon #MagoliYaSimbaVsAfricanLyon #Simba #AfricanLyon #AdamSalamba #JohnBocco #JohnBoco

Baada ya Mechi ya JKT Tanzania vs Yanga SC, Msimamo kwa Yanga huu
Baada ya Mechi ya JKT Tanzania vs Yanga SC, Msimamo kwa Yanga huu

Baada ya Mechi ya JKT Tanzania vs Yanga SC, Msimamo kwa Yanga huu. JKTtanzaniaVsYanga #YangaNaJktTanzania #LigiKuuTanzaniaBara #TanzaniaPremierLeague #SisiNiSoka #AzamTVApp #JktTanzania #YangaSC #AllianceFC #KMC #Msimamo #MsimamoWaLigi #Standing #LeagueTable

AZAM FC 1-1 ALLIANCE FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 6/2/2019)
AZAM FC 1-1 ALLIANCE FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 6/2/2019)

Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali. Mchezo huo ulikuwa na kasi sana, Azam FC ikianza kwa mashambulizi makali langoni mwa Alliance, ambapo dakika ya kwanza Obrey Chirwa, alikosa bao la wazi baada ya kuupiga vibaya mpira akiwa anatazamana na lango ndani ya eneo la hatari, akipokea pasi ya Donald Ngoma. Mabingwa hao waliweza kupata ugumu kuipenya safu ya ulinzi ya Alliance, kutokana na timu hiyo kusimama wengi kujilinda nyuma ya mpira wakati Azam FC ikishambulia. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, kipa wa Azam FC, Razak Abalora, alioneshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano iliyosababishwa na lugha ya kutoridhishwa na maamuzi aliyoitoa kwa mwamuzi huyo. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 48 katika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ikizidiwa pointi saba na kinara Yanga aliyefikisha 55 kufuatia suluhu yake ya jana dhidi ya Singida United.

ALLIANCE FC 2-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 02/02/2019)
ALLIANCE FC 2-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 02/02/2019)

Timu ya Alliance FC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Nyamagana jijini Mwanza. Magoli ya Alliance yote mawili yamepatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa Dickson Ambundo dakika ya 9 na Juma Nyange dakika ya 30. Ushindi huo umeifanya Alliance kusogea hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 31 nyuma ya Mbao FC na Lipuli FC ambao wote wana pointi 33.

YANGA SC 3-1 MWADUI FC HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL-15/1/2019)
YANGA SC 3-1 MWADUI FC HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL-15/1/2019)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC wameendeleza ubabe wao kwenye ligi hiyo msimu huu baada ya leo kuiadhibu Mwadui Fc kwa kipigo cha mabao 3-1, mchezo ukipigwa kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Ajibu kwa ‘free-kick’ dakika ya 12, Amissi Tambwe dakika ya 39 akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu na Feisal Salum kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 58 huku bao la kufutia machozi la Mwadui likifungwa na Salim Aiyee dakika ya 82. Mbali na kupatikana kwa mabao hayo, Ibrahim Ajibu alikosa mkwaju wa penati iliyopanguliwa na golikipa wa Mwadui FC Anold Masawe dakika ya 19. Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 53 na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi huku wanaowafuatia Azam Fc wakiwa na pointi 40 na mchezo mmoja mkononi.

MAGOLI YOTE: YANGA SC 3-1 MWADUI FC (TPL – 15/01/2019)

« Previous Next »

Popular Tags

#Kawhi Leonard  #Zlatan Ibrahimovi  #Paul Pogba  #Zlatan Ibrahimovi  #Gareth Bale  #Goalkeeper Saves  #Best Goals Ever  #Mesut Ozil  #Derrick Rose  #Luis Suarez  

Popular Users

#steveaustinBSR  #TheChristinaKim  #si_vault  #Oprah  #CP3  #RobGronkowski  #twitter  #DjokerNole  #cesc4official  #ArianaGrande  #sportspickle  #SHAQ  #TheRealJRSmith