Kikosi cha Yanga SC kimefanya mazoezi yao ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya Mchezo wa Februari 24,2024 wa ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya CR Belouizdad,Utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa,Saa 1:00 jioni.
Leo Februari 20,2024 Yanga SC inaialika Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex Chamazi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports,Saa 1:00 Jioni.
Leo Februari 17,2024 KMC FC inashuka Dimba la Jamhuri Morogoro kuikaribisha Yanga SC katika mchezo wa ligu kuu ya NBC,Saa 10:00 Jioni. Kaa karibu na Mpenja TV kupata taarifa zote za kabla na baada ya mchezo huo.
Kikosi cha Simba SC,kimerejea Jijini Dar es salaam leo Februari 13,2024 kikitokea Jijini Mwanza baada ya kucheza michezo minne ya ligi kuu ya NBC katika Mikoa Mitatu,Februari 3 dhidi ya Mashujaa FC Kigoma,Februari 6 dhidi ya Tabora United, Tabora,Februari 9 dhidi ya Azam FC Mwanza na Februari 12 dhidi ya Geita Gold Mwanza. Kwenye Michezo hiyo Minne Simba SC imevuna Alama 10 kati ya 12,imemfunga Mashujaa FC 1-0,Ikamfunga Tabora United 4-0,Ikatoka Sare ya 1-1 na Azam FC na ikamfunga Geita Gold 1-0.
Leo Februari 10,2024 Klabu ya Yanga imefanya Wananchi Mbeya Jogging ikiwa ni Sherehe za maadhimisho ya miaka 89 ya Klabu hiyo,Zinazofanyika Jijini Mbeya. Pia wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya,Kitengo cha Wazazi na Magonjwa ya Wanawake Meta, kuwajulia hali Wagonjwa na kuwapatia Zawadi mbalimbali.
Leo Februari 5,2024 Yanga SC inashuka Dimba la Azam Complex chamazi kumenyana na Dodoma Jiji FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC,Saa 1:00 Usiku.
Leo Januari 31,2024 Simba SC inashuka Dimba la Azam Complex chamazi kumenyana na Tembo SC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports,Saa 1:00 Usiku.