Stephane Aziz Ki amefunga #hattrick ... Yanga ikiitandika KMC mabao 6-1 kwenye dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya NBC. Hat-trick ya Aziz Ki imepatikana kwa penati mbili dakika za 18 na 56, huku lingine lingia nyavuni dakika ya 49. Aliyefungua mlango wa magoli ni Prince Dube dakika ya 10... huku Maxi Nzengeli na Israel Mwenda nao wakifunga dakika za majeruhi... Bao la kufutia machozi limetoka kwa Redemtus Mussa dakika ya 51. Haya hapa magoli yote...
Magoli matatu yote kipindi cha kwanza… Simba inaipiga Tanzania Prisons 3-0 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam. Wafungaji ni Jean Charles Ahoua, Elie Mpanzu na Ladack Chasambi. Hii ni Ligi Kuu ya NBC 2024-25
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya NBC Premier League kati Tabora United dhidi ya Simba SC. Simba imeshinda kwa jumla ya magoli 3-0, Magoli yamefungwa na Leonel Ateba na Shomari Kapombe
#MakarashaDay: Tazama ‘vimbwanga’ vya Bernard Morrison baada ya kutambulishwa ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya ikiwa ni ingizo jipya kwenye kikosi cha KenGold. Wchezaji wengine waliotambulishwa ni pamoja na Morrison ni Kelvin Yondani na Obrey Chirwa. #MakarashaDay #KenGold #HashukiMtu #AzamSports1HD
Tazama magoli yote sita waliyofunga Simba SC kwenye mchezo wa hatua ya 64 bora ya CRDB Bank Federation Cup Simba imeshinda kwa jumla ya magoli 6-0, wafungaji ni Valentino Mashaka, Ladack Chasambi, Joshua Mutale, Stephen Mukwala, Edwin Balua na goli la kujifunga la Patrick Sebastian
Tazama magoli yote matano ya Yanga waliyofunga kwenye mchezo wa CRDB Bank Federation Cup dhidi ya Copco FC. Wafungaji ni Shekhan Ibrahim, Prince Dube, Maxi Nzengeli, Duke Abuya na Mudathir Yahya.
#TWPL Tazama magoli ya Simba SC yaliyopatikana ndani ya dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2025 kati ya Mlandizi Queens dhidi Simba Queeens; huku Asha Djafari na Jentrix Shikangwa... wakipiga Hat-trick katika mchezo huo. #TanzaniaWomensPremierLeague #LigiKuuWanawake #TWPLUpdates #MlandiziQueens #SimbaQueens #MlandiziSimba
Timu ya taifa ya Zanzibar… #ZanzibarHeroes imeibuka na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025 kwa kuichapa Burkina Faso mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa leo kwenye Dimba Gombani, Pemba. Zanzibar walitangulia kupata bao dakika ya 41 kwa kisigino cha Ibrahim Hamad Hilika, kisha Burkina Faso wakachomo dakika ya 69 kupitia kwa Aboubacar Traore…. Lakini dakika za majeruhi, Hassan Ali Cheda akafunga la pili na la ushindi kwa Zanzibar.