Magoli mawili ya Emmanuel Keyekeh na moja la Jonathan Sowah yameipa ushindi wa 3-1 Singida Black Stars dhidi ya Simba na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank. Ni katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa kwenye Dimba la Tanzanite Kwaraa, Babati Manyara ambapo Simba imepata goli lake la kufutia machozi kupitia kwa free-kick ya Jean Charles Ahoua. Kwa matokao haya, safari ya Simba imeishia hapa.... na Singida BS wanakwenda fainali kuwakabili Yanga...
Steven Mukwala amefunga goli pekee na la ushindi kwa Simba, dhidi ya Singida Black Stars, mchezo wa Ligi Kuuya NBC uliopigwa kwenye Dimba la KMC, Mwenge Dar es Salaam.
Yanga imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank kwa kuichapa JKT Tanzania mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa Mkwakwani Stadium, jijini Tanga.... Magoli ya Yanga kwenye mchezo huu yamefungwa na Prince Dube dakika ya 41 na Mudathir Yahya dakika ya 90.
Jean Charles Ahoua amepiga hattrick Simba ikiinyuka Pamba Jiji FC kichapo cha mabao 5-1 kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Ahoua amefunga magoli yake dakika ya 16' kwa penati, 37' na 48' huku mawili yakifungwa na Lionel Ateba Mbida dakika ya 80 na 84. Goli pekee la kufutia machozi kwa Pamba limefungwa na Mathew Momanyi Tegis dakika ya 86....
Fabrice Ngoma amefunga goli pekee lililowapa Simba ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya JKT Tanzania, mchezo wa ligi kuu ya NBC ukipigwa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam.
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo wa NBC Premier League kati ya Simba SC dhidi ya Mashujaa FC. Simba imeshinda kwa jumla ya magoli 2-1. Magoli ya Simba yamefungwa na Leonel Ateba kwa mikwaju ya penati. Goli la Mashujaa limefungwa na Jafary Kibaya
#MuunganoCup2025: Tazama golikipa wa Yanga SC, Abuutwalib Mshery alivyoonesha umahiri wake katika kupangua mikwaju ya penati. Fainali ni JKU dhidi ya Yanga SC, Alhamisi Mei 1, 2025 saa 1:15 usiku FT’: Zimamoto 1-1 Yanga SC (Pen:1-3) #TanzaniaUnionSuperLeague #TUSL #MuunganoCup2025 #MuunganoCup #KombeLaMuungano #SuperLeague #YeNaniAsife #Zimamoto #YangaSC #ZimamotoYanga
Tazama matukio yote makubwa yaliyojiri kwenye mchezo kati ya KVZ dhidi ya Yanga SC kwenye Muungano Cup Yanga imeshinda kwa jumla ya magoli 2-0 Wafungaji ni Stephane Aziz Ki na Denis Nkane