KUTOKA MISRI: Kikosi cha Simba kilichopo Misri, katika maandalizi ya msimu mpya wa NBC Premier League na mashindano ya kimataifa, kimecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Carabat FC, ambapo Mnyama ameshinda magoli 2-0. Goli la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Mohammed Bajaber huku goli la pili likifugwa kipindi cha pili na Jonathan Sowah. Wachezaji wote wawili wamesajiliwa msimu huu. #Simba #KambiYaSimba
KUTOKA MISRI | “….hakuna kiumbe yeyote anayeweza kujiita Eliiiii zaidi ya Simba SC” Kikosi cha Simba SC kikiwa kambini nchini Misri, jioni ya leo kimepiga tizi lililomuhusisha pia kiungo wao Elie Mpanzu ambaye ameripoti kambini hapo leo… Katika tizi hizo hilo, meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyemamu amefafanua machache kuhusu utata uliokuwepo juu ya mchezaji huyo, akisema “…ni propaganda…ni Gen-z ambao wameingia kwenye mfumo wa kisasa wa mpira” Rweyemamu amesema klabu hiyo haiwezi kufanya makosa ya kumsajili mchezaji wa aina hiyo kwa mkataba wa miezi sita na kusisitiza kuwa “…Elie Mpanzu yupo, na ataendelea kuwepo hadi Simba itakavyoamua vinginevyo
Goli pekee la Idd Selemani 'Nado' limeipa Tanzania #TaifaStars pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda, katika mchezo wa ufunguzi wa michuano maalum ya CECAFA 3 Nations Tounarment #CECAFA3NT inayopigwa kwenye Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha...
“…tuliweka kiwango kizuri cha fedha kumshawishi mchezaji na klkabu yake” Nneno la Ally Kamwe kuhusu usajili wa kiungo Moussa Balla Conte ambaye leo ametua rasmi Jangwani kwa mkataba wa miaka mitatu… Kamwe ameeleza jinsi ilivyokuwa ngumu kumpata na jinsi walivyoweza kumshawishi yeye na klabu yake licha ya kuwa na ofa nyingi….. Kuhusu hatma ya Khalid Aucho, Kamwe amesema majibu yatatoka Julai 20 baada ya kupokea ripoti ya CEO wa klabu hiyo… Mwisho, Ally Kamwe anatoa ujumbe kwa walioumizwa na usajili huo akiomba kusajiliwa na timu inayohitaji mchezaji mwenye jina la Conte…. #YangaSC #Usajili #BallaConte
KARIAKOO DERBY | Magoli ya Pacome Zouzoua kwa penati na Clement Mzize yameipa Yanga pointi tatu muhimu dhidi ya mtani wake Simba SC na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2024/25 baada ya kufikisha alama 82 dhidi ya 78 za Simba... Huu ulikuwa ni mchezo wa mwisho wa msimu ambao pia ulikuwa ukisubiriwa kutoa maamuzi ya nani awe bingwa wa ligi hii msimu huu... Mbungi imepigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Itazame Dar es Salaam, itazame Benjamin Mkapa, watazame watani wa jadi…!!! #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #KariakooDerby #DabiYaKariakoo #HainaKipengele #YangaSC #SimbaSC #YangaSimba #WataniWaJadi
Yanga SC imeichakaza Tanzania Prisons kwa kichapo cha mabao 5-0 kwenye mchezo wa raundi ya 29 Lig kuu ya NBC uliopigwa Sokoine Stadium, Mbeya... Pacome Zouzoua amefunga magoli mawili, huku mengine yakitoka kwa Mudathir Yahya aliyefungua milango dakika ya 31, Clatous Chama, na Israel Mwenda..