MAGOLI: AZAM FC 1-1 ALLIANCE FC (TPL – 06/02/2019)
MAGOLI: AZAM FC 1-1 ALLIANCE FC (TPL – 06/02/2019)

Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali.



AZAM FC 1-1 ALLIANCE FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 6/2/2019)
AZAM FC 1-1 ALLIANCE FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 6/2/2019)

Azam FC, imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ilibidi Azam FC iweze kusubiri hadi dakika ya 79 kuweza kupata bao la uongozi, lililofungwa na Joseph Mahundi, aliyeingia dakika ya 76, kuchukua nafasi ya Ramadhan Singano, na alifunga bao hilo kiustadi akiunganisha krosi ya Chirwa. Dakika ya 90 Alliance ilisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo, akimalizia mpira uliogonga mwamba kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Israel Patrick. Azam walionekana kulalamikia bao hilo wakidai kuwa beki wao Agrey Moris alisukumwa kabla ya kufungwa lakini, mwamuzi Abubakar Mturo (Mtwara) na Msaidizi namba moja, Mohamed Mkono (Tanga), waliamuru kuwa bao halali. Mchezo huo ulikuwa na kasi sana, Azam FC ikianza kwa mashambulizi makali langoni mwa Alliance, ambapo dakika ya kwanza Obrey Chirwa, alikosa bao la wazi baada ya kuupiga vibaya mpira akiwa anatazamana na lango ndani ya eneo la hatari, akipokea pasi ya Donald Ngoma. Mabingwa hao waliweza kupata ugumu kuipenya safu ya ulinzi ya Alliance, kutokana na timu hiyo kusimama wengi kujilinda nyuma ya mpira wakati Azam FC ikishambulia. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, kipa wa Azam FC, Razak Abalora, alioneshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano iliyosababishwa na lugha ya kutoridhishwa na maamuzi aliyoitoa kwa mwamuzi huyo. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 48 katika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ikizidiwa pointi saba na kinara Yanga aliyefikisha 55 kufuatia suluhu yake ya jana dhidi ya Singida United.



ALLIANCE FC 2-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 02/02/2019)
ALLIANCE FC 2-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 02/02/2019)

Timu ya Alliance FC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Nyamagana jijini Mwanza. Magoli ya Alliance yote mawili yamepatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa Dickson Ambundo dakika ya 9 na Juma Nyange dakika ya 30. Ushindi huo umeifanya Alliance kusogea hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 31 nyuma ya Mbao FC na Lipuli FC ambao wote wana pointi 33.



HIGHLIGHTS: ALLIANCE FC 1-0 MTIBWA SUGAR (TPL – 07/11/2018)
HIGHLIGHTS: ALLIANCE FC 1-0 MTIBWA SUGAR (TPL – 07/11/2018)

Vijana wa Alliance FC leo wamewachapa wakongwe Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Bao pekee la Alliance limefungwa na Dickson Ambundo dakika ya 54 akimalizia pasi ya Michael Chinedu baada ya kipa wa Mtibwa Shaaban Kado kuutema mpira uliopigwa na Siraji Juma. Katika mchezo huo, Alliance imetawala zaidi mchezo pamoja na kufanya mashabulizi zaidi kuliko Mtibwa huku ikionekana kujiimarisha zaidi katika safu yake ya ulinzi na kudhibiti mashambulizi ya Mtibwa yaliyoongozwa na Juma Luizio, Kelvin Sabato, Ismail Mhesa na Salum Kihimbwa. Matokeo hayo yanaifanya Alliance kufikisha pointi 13 na kukaa nafasi ya 16 wakati Mtibwa ikiendelea kukaa nafasi ya nne ikiwa na pointi 23.



Alliance FC 1-0 Mtibwa Sugar; Bao pekee la Alliance (TPL - 07/11/2018)
Alliance FC 1-0 Mtibwa Sugar; Bao pekee la Alliance (TPL - 07/11/2018)

Vijana wa Alliance FC leo wamewachapa wakongwe Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Bao pekee la Alliance limefungwa na Dickson Ambundo dakika ya 54 akimalizia pasi ya Michael Chinedu baada ya kipa wa Mtibwa Shaaban Kado kuutema mpira uliopigwa na Siraji Juma.



Magoli Yote: SIMBA 5 -1 ALLIANCE FC, LIGI KUU, 24 OKT 2018
Magoli Yote: SIMBA 5 -1 ALLIANCE FC, LIGI KUU, 24 OKT 2018

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars OKWI, CHAMA, KWASI NA SALAMBA WOTE WAFUNGA SIMBA SC YAIKANDAMIZA ALLIANCE FC 5-1 TAIFA MABINGWA watetezi, #SimbaSC wamepata ushindi wa kishindo baada ya kuichapa 5-1 #AllianceFC katika mchezo wa #LigiKuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikiziwa pointi nne na vinara, Azam FC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi. Watani wao wa jadi, Yanga SC wanafuatia kwa pointi zao 19 na kesho watacheza mechi yao ya nane kwa kumenyana na KMC Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa. Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi alifunga bao la kwanza dakika ya 10 kwa kichwa akimalizia pasi ya kocha baada ya krosi ya beki Mghana, Nicholas Gyan baada ya kona fupi kutoka upande wa kulia. Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan/Shomari Kapombe dk46, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Pascal Wawa, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Hassan Dilunga dk61, Clatous Chama, Adam Salamba/Meddie Kagere dk75, John Bocco na Emmanuel Okwi. Alliance FC; Kelvin Richard, Israle Patrick, Hance Masoud, Wema Sadock, Geoffrey Luseke, Juma Nyangi, Dickson Ambundo, Balama Mapinduzi/Martin Kiggi dk89, Michael Chinedu/Juhudi Philemon dk61, Jamal Mtegeta/Zabona Khamis dk80 na Siraj Juma. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars




« Previous


Popular Tags

#Derrick Rose  #Lionel Messi  #Sergio Aguero  #Zlatan Ibrahimovi  #Shot Goals  #Best Ball Controls  #Michael Jordan  #Best Goalkeeper Saves  #Cristiano Ronaldo  #Kawhi Leonard  

Popular Users

#BellaTwins  #jadande  #ddlovato  #kevinlove  #Harry_Styles  #baseballpro  #cesc4official  #JLo  #DeAndre  #BillGates  #TimTebow  #RealSkipBayless  #rihanna  #BadgerMBB  #Oprah