Timu ya Alliance FC imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Nyamagana jijini Mwanza. Magoli ya Alliance yote mawili yamepatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa Dickson Ambundo dakika ya 9 na Juma Nyange dakika ya 30. Ushindi huo umeifanya Alliance kusogea hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 31 nyuma ya Mbao FC na Lipuli FC ambao wote wana pointi 33.