Vijana wa Alliance FC leo wamewachapa wakongwe Mtibwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Bao pekee la Alliance limefungwa na Dickson Ambundo dakika ya 54 akimalizia pasi ya Michael Chinedu baada ya kipa wa Mtibwa Shaaban Kado kuutema mpira uliopigwa na Siraji Juma.