Ilikuwa ni funga nikufunge, Simba ikitangulia, kisha kutokea nyuma na kushinda mechi dhidi ya Namungo FC, mchezo ukipigwa kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Anicet Oura amefunga mawili huku lingine likifungwa na Rushine de Reuck kwa penati wakati magoli mawili ya Namungo yakitoka kwa Raymond Lulendi.