Azam TV's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Magoli kutoka kwa Israel Patrick Mwenda, Clement Mzize na Prince Dube yameipa Yanga ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC ukipigwa kwenye Dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Hiki ni kisasi kwa Yanga dhidi ya Tabora United, ikikumbkwa mchezo wa kwanza waliokutana msimu huu, Yanga ilipoteza nyumbani kw akichapo cha mabao 3-1 kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.
Ni mechi ya kirafiki iliyoshindwa kumalizika baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha mjini Singida na mechi kuahirishwa ikiwa imechezwa kwa dakika 57 pekee. Hadi muda huo, ubao ulikuwa ukisomeka 1-1, wakianza Yanga dakika ya kupitia kwa Jonathan Ikangalombo na kisha Singida kusawazisha dakika ya 56 kupitia kwa Marouf Tchakei. Ni Singida Black Stars dhidi ay Yanga, mchezo maalum wa kuzindua Uwanja mpya wa Airtel unaomilikiwa na klabu ya Singida Black Stars. Haya hapa magoli…
Simba SC imeipa kichapo cha mabao 6-0 Dodoma Jiji FC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la KMC, Dar es Salaam. Elie Mpanzu ndiye aliyeitanguliza Simba dakika ya 16 na kisha Jean Charles na Kibu Denis wakafunga mawili kila mmoja huku linguine likiwekwa nyavuni na Steven Desse Mukwala…
Yanga SC imeichapa Coastal Union mabao 3-1 na kutinga 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank, mchezo ukipigwa kwenye Dimba la KMC Complex. Maxi Nzengeli amefunga magoli mawili dakika ya 2 na 15, wakati Clement Mzize akipiga la tatu dakika ya 21 baada ya Coastal Union kupata bao la dakik aya 18 kupitia kwa Miraji Abdallah. Magoli yote yamefungwa ndani ya dakika 21 za kwanza….
Magoli matatu yamefungwa, Simba ikipenya kuingia 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank kwa kuifunga TMA Stars mabao 3-0 kwenye Dimba la KMC Complex. Magoli ya Simba yamefungwa na Valentine Nouma, Sixtus Sabilo kwa kujifunga na Lionel Ateba..... Kwa kuvuka hatua hii, Simba sasa itakutana na Bigman FC kwenye hatua hiyo...
HATTRICK: Steven Desse Mukwala amefunga hattrick, Simba ikiitandika Coastal Union mabao 3-0 kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid Arusha, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara. Mukwala amefunga magoli yote matatu dakika ya 30, 45 na 56 Tazama highlights...
MZIZIMA DERBY | Ni sare ya 2-2 kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC, uliopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Azam wametangulia kwa goli la Gibril Sillah dakika ya 01, kabla ya Elie Mpanzu kusawazisha dakika ya 25 na Abdulrazak Hamza kuongeza la pili dakika ya 76. Nyota wa mchezo ni ‘Super Sub’, Zidane Sereri ndiye aliyeweka mambo sawa kwa kuifungia Azam FC bao la kusawazisha dakika ya 88, kwa assist ya aina yake kutoka kwa Feisal Salum Feitoto.
Clatous Chama amefunga magoli mawili, Yanga ikiichakaza Mashujaa FC magoli 5-0 kwenye Dimba la Lake Tanganyika, Kigoma, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.... Chama amefunga dakika ya 74 na 83 huku mengine yakifungwa na Duke Abuya, Prince Dube na Khalid Aucho..
Tazama matukio na Magoli yote mawili.... Aliyeanza ni Bright Adjei na aliyejibu ni Pius Buswita. FT: Namungo 1-1 Singida BS.
Tazama highlights za mechi kati ya Azam FC dhidi ya Polisi Tanzania ambapo vijana wa Chamazi wameleka kilio cha mabao 8-0 ...
Magoli mawili ya Singida Big Stars…. Wauaji ni Bruno Gomes na Medie Kagere… .
Haya hapa magoli ya Ihefu ikiibamiza Geita Gold kwenye mchezo wa mzunguko wa 39 NBC Premier League. FT: Ihefu SC 3-0 ...
Fiston Mayele amefunga la kwanza dakika ya 33 na Yannick Bangala akitokea benchi akafunga la pili dakika ya 90, Yanga ...
Simba imeichapa Coastal Union mabao 3-1 katika mchezo wa kuhitimisha msimu 2022/23 uliopigwa kwenye dimba la Uhuru, ...
Magoli mawili kutoka kwa Rashid Juma na Obrey Chirwa (penati) yameipa ushindi wa mabao 2-0 Ihefu SC dhidi ya Kagera Sugar ...
MBEYA CITY 0-1 KMC: Ni Deogratius Anthony aliyewashtukiza Mbeya City kwa kuwadunga bao goli la sekunde ya 35 baada ya ...