Azam TV's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Zimepigwa penati tatu, Simba ikiitandika Namungo FC mabao 3-0 kwenye Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Jean Charles Ahoua amefunga penati mbili, huku Lionel Ateba akikosa penati moja iliyookolewa na golikipa wa Namungo, Jonathan Nahimana. Goli la tatu kwa Simba limefungwa na Steven Mukwala dakika za majeruhi... Katika mchezo huu pia, Namungo wamepata pigo baada ya beki wake Derrick Mukombozi kutolewa kwa kadi nyekundu...
Yanga SC imeendeleza ubabe kwenye ligi, kwa kumchapa Singida Black Stars mabao 2-1 kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Waliofunga magoli ya Yanga ni Clement Mzize dakika ya 14 na Prince Dube dakika ya 43 wakati Jonathan Sowah akifunga goli pekee la kufutia machozi... Hii ni Ligi Kuu ya NBC #NBCPremierLeague
Stephane Aziz Ki amefunga #hattrick ... Yanga ikiitandika KMC mabao 6-1 kwenye dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya NBC. Hat-trick ya Aziz Ki imepatikana kwa penati mbili dakika za 18 na 56, huku lingine lingia nyavuni dakika ya 49. Aliyefungua mlango wa magoli ni Prince Dube dakika ya 10... huku Maxi Nzengeli na Israel Mwenda nao wakifunga dakika za majeruhi... Bao la kufutia machozi limetoka kwa Redemtus Mussa dakika ya 51. Haya hapa magoli yote...
Magoli matatu yote kipindi cha kwanza… Simba inaipiga Tanzania Prisons 3-0 kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam. Wafungaji ni Jean Charles Ahoua, Elie Mpanzu na Ladack Chasambi. Hii ni Ligi Kuu ya NBC 2024-25
Simba SC imekabwa koo na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Tanzanite, Kwaraa, Babati Manyara... Simba wametangulia kupata bao kupitia kwa Lionel Ateba dakika ay 57 lakini kiungoLadack Chasambi akajifunga na kuisawazishia Fountain Gate dakika ya 75. Katika mchezo huu pia, Fountain Gate ilipata pigo kwa golikipa wake John Noble kutolewa kwa kadi nyekundu, ikiwa ni njano ya pili....
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya NBC Premier League kati Tabora United dhidi ya Simba SC. Simba imeshinda kwa jumla ya magoli 3-0, Magoli yamefungwa na Leonel Ateba na Shomari Kapombe
#MakarashaDay: Tazama ‘vimbwanga’ vya Bernard Morrison baada ya kutambulishwa ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya ikiwa ni ingizo jipya kwenye kikosi cha KenGold. Wchezaji wengine waliotambulishwa ni pamoja na Morrison ni Kelvin Yondani na Obrey Chirwa. #MakarashaDay #KenGold #HashukiMtu #AzamSports1HD
Tazama magoli yote sita waliyofunga Simba SC kwenye mchezo wa hatua ya 64 bora ya CRDB Bank Federation Cup Simba imeshinda kwa jumla ya magoli 6-0, wafungaji ni Valentino Mashaka, Ladack Chasambi, Joshua Mutale, Stephen Mukwala, Edwin Balua na goli la kujifunga la Patrick Sebastian
Mkwaju wa penati kutoka aliopigwa na Raizin Hafidh ndiyo uliowapa ushindi Dodoma Jiji FC dhidi ya Ruvu Shooting, mechi ya ...
Mtibwa Sugar imeitandika Geita Gold FC mabao 3-1 na kubaki salama ndani ay #NBCPremierLeague baada ya kuhitimisha ...
Tazama magoli yote mawili... Aliyeanza ni Bright Adjei dakika ya 69 na aliyejibu ni Pius Buswita dakika ya 79. Namungo ikatoika ...
Prince Dube amefunga magoli manne dakika ya 8, 15, 28 na 56; Idd Nado akifunga mawili dakika ya 40 na 75, Kipre Jr. goli lake ...
Fiston Mayele amefunga la kwanza dakika ya 33 na Yannick Bangala akitokea benchi akafunga la pili dakika ya 90, Yanga ...
Simba imeichapa Coastal Union mabao 3-1 katika mchezo wa kuhitimisha msimu 2022/23 uliopigwa kwenye dimba la Uhuru, ...
Shughuli inafanyika kwenye Dimba la Sokoine jijini Mbeya baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa ushindi ...
Tazama kipindi cha Mshikemshike Viwanjani ikiwa na habari kemekem ikiwemo utambulisho wa Feisal Salum ndani ya Azam FC ...