Mwananchi Digital's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Alichozungumza Msemaji na Mhasishaji wa klabu ya Yanga Antony Nugaz baada ya Mchezo wao dhidi ya Biashara United ya mkoani Dodoma leo kwenye uwanja wa Benjamin mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa bao moja kwa bila.
Kutana na mtoto Fathiya shabiki kindakindaki wa Simba SC ambaye ametabili matokeo ya Simba na kweli alichokitabili kimetimia.
Tazama kilichotekea baada ya gari lilokuwa limewabeba wachezaji wa klabu ya Simba kutoka nje ya uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya mchezo wa hatua ya makundi klabu bingwa Afrika kati ya Simba Sc dhidi ya Al Merreikh ya Sudan.
Mashabiki wa Simba wakati wakiwa wanasubiria gari la timu yao litoke uwanja wa Benjamin Mkapa hili waweze kuwapongeza wachezaji baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Al Merreikh ya sudan mchezo wa hatua ya makundi mabingwa Afrika.
Msikilize shabiki huyu wa klabu ya Simba akiizungumzia klabu yake baada ya kumaliza kifua mbele wa kuifunga bao tatu dhidi ya klabu ya Al Merreik ya Sudan leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kudai kuwa Al Merreikh walikuwa wafungwe 15 badala ya tatu.
Mashabiki wa klabu ya Simba waliokuwa nje kidogo ya uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye eneo la bar, baada ya mchezo wao dhidi ya Al Merreikh kumalizika waliibuka na kudai kuwa klabu hiyo kutoka Sudan imefungwa kwasabu ya rangi ya Jezi waliyotumia kwenye mchezo huo.
Tazama mashabiki wa klabu ya simba walio jitokeza bar nje kidogo ya uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa wanafuatilia mchezo wao dhidi ya Al Merreikh.
Maneno ya Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Cedric Kaze baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania kunako dimba la Sheikh Amri Abeid Arusha .