Mwananchi Digital's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Golikipa wa Mwadui FC akizungumza baada ya Mchezo wao dhidi ya Yanga SC, amesema katika mchezo wa leo alipanaga yanga wasipate goli lakini haikuwa bahati.
Wasikie mashabiki wa klabu ya Simba waliopo jijini Mwanza kuhuhudia mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania FC, mchezo utakao pigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Sikiliza alichokisema Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz kuhusu makosa ya kimichezo yaliyofanywa na kipa namba moja wa klabu hiyo Metacha Mnata, kwenye mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting,
Wasikie Mashabiki wa Taifa Stars waliojitokeza Baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa timu za taifa kumalizika katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, kati Tanzania dhidi ya na Malawi, mchezo uliomalizika kwa Tanzania kumfunga Malawi goli mbili kwa bila.
Tazama tukio hili la Wabunge kumkaribisha Mchezaji wa kimataifa wa timu ya Crystal Palace ya Uingereza na timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho, baada ya kutambulishwa bungeni wakati kikao cha 41 cha Bunge la Bajeti kilipokuwa kikiendelea jijini Dodoma leo.
Tazama Pambano lote la Bondia Hassan Mwakinyo wa Tanzania dhidi ya Antonio Mayala Bondia kutokea Angola.
Uchambuzi wa mchezo wa robo fainali ya pili ya ligi ya mabigwa afrika kati ya Simba SC dhidi ya Kaizer Chiefs FC, mchezo utakao pigwa kunako dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 10:00 za jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Sikiliza walichokisema baadhi ya mashabiki wa klabu ya Simba Sc walijitokeza kuutazama mchezo wa ligi kuu leo kati ya Yanga dhidi ya Azam na kushuhudia mchezo huo ukimalizika kwa Yanga kupoteza kwa bao moja bila.