Dream Online Tv's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
@LuisMiquissone pulled off some stunning performances with @SimbaSCTanzania last season! #TotalEnergiesCAFCL
HII NDIO KAULI YA ADEN RAGE|BAADA YA MANARA KUHAMIA YANGA|"YEYE SIO LOLOTE" Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Ismail Aden Rage amesema @HajiManara hakuwa kiongozi ndani ya timu hiyo na badala yake alikuwa ni mwajiriwa na mpiga porojo hivyo hajachukia kuondoka kwake kwa sababu kwa kazi yake anaruhusiwa kwenda timu yeyote huku akimuonya kutoikashifu Simba.
AFISA HABARI WA SIMBA SC|ASEMA WANATANGAZA VYUMA VITATU|KUACHANA NA KAGERE|WAINGIA KAMBINI RASMI
KAIMU AFISA HABARI WA SIMBA ASEMA LEO WANATANGAZA CHUMA KIPYA CHA KIGENI|Wanaingia Kambini Jumapili
Kuna faida nyingi Simba ikimuuza Miquissone Al Ahly . . Nimeona mijadala na taarifa nyingi zinaendelea kuhusu Luis Miquissone.. Inasemekana kuna timu nyingi kubwa kutoka nje zinamhitaji.. Inapendeza sana.. . Nasikia kuna ofa inayofikia Bilioni 1.6 imetolewa na Al Ahly ya Misri kwa Miquissone.. Ni pesa nyingi sana.. Inatokea mara chache kwa mchezaji kutoka Ligi ya Tanzania akauzwa pesa nyingi hivyo.. . Ilitokea kwa Okwi miaka mingi nyuma.. Aliuzwa Dola 300,000 (Mil 450 kwa wakati huo)... Bahati mbaya Simba ililazimika kuisubiri pesa hiyo kwa miaka mitatu.. . Tofauti na Okwi, hakuna mchezaji mwingine kutoka Ligi ya Tanzania amewahi kuuzwa zaidi ya Milioni 300.. Hivyo ofa ya Miquissone ni rekodi mpya kwa soka letu.. . Hata hivyo inadaiwa kuwa Simba bado haijawa tayari kumuuza Miquissone.. Wanadai kuwa malengo yao Afrika ni makubwa hivyo wanadhani si muda sahihi kumuuza nyota wao.. . Lakini kwa mtazamo wangu Simba ingekubali tu kumuuza Miquissone.. Kuna faida nyingi katika biashara hiyo. . Kwanza katika biashara hiyo, Simba itapiga pesa.. Usajili wa Miquissone haukugharimu zaidi ya dola 200,000 lakini leo Simba inamuuza kwa Dola 700,000.. Ni faida kubwa.. . Ni mchezaji gani mwingine Simba inaweza kumuuza kwa faida kubwa hivyo? Hakuna. Siyo Chama wala Bwalya.. . Pili, kwa kumuuza Miquissone kwenda klabu kubwa Afrika itavutia wachezaji wengi zaidi kwenda Simba.. Wataona Simba ni daraja la mafanikio.. . Simba itakuwa na heshima yake kwenye soko la usajili.. Wachezaji wengi wenye ndoto kama za Miquissone watatamani kwenda Simba. Vipi Simba ikigoma kumuuza? Wachezaji wakubwa wataona Simba siyo timu nzuri ya kuwafikisha wanapotaka.. . Asikwambie mtu, hakuna mchezaji yoyote mkubwa Afrika hatamani kucheza Al Ahly, Wydad Club au Mamelodi Sundowns.. Ndio timu za ndoto za wengi..
MIQUISSONE SITUATION Al Ahly Tayari wamefanya mazungumzo na Miquissone na kufikia makubaliano,Miquissone anavutiwa sana kucheza chini ya Pitso Mosimane ambae waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Mamelodi Sundowns! Ofa ya Tshs 2 billion inatarajiwa kutolewa na Al Ahly kwenda Simba Kaizer Chiefs wao wamejitoa rasmi kwenye mbio za kumsajili Miquissone hawako tayari kutoa ada ya uhamisho inayotakiwa na Simba,Pia mchezaji mwenyewe hayuko tayari kujiunga na Kaizer Chief Simba wao Tayari wanamtazama Moses Phiri 🇿🇲 Kama mbadala wa Miquissone #TanzaniaTransfer #SimbaSc🦁