Kuna faida nyingi Simba ikimuuza Miquissone Al Ahly . . Nimeona mijadala na taarifa nyingi zinaendelea kuhusu Luis Miquissone.. Inasemekana kuna timu nyingi kubwa kutoka nje zinamhitaji.. Inapendeza sana.. . Nasikia kuna ofa inayofikia Bilioni 1.6 imetolewa na Al Ahly ya Misri kwa Miquissone.. Ni pesa nyingi sana.. Inatokea mara chache kwa mchezaji kutoka Ligi ya Tanzania akauzwa pesa nyingi hivyo.. . Ilitokea kwa Okwi miaka mingi nyuma.. Aliuzwa Dola 300,000 (Mil 450 kwa wakati huo)... Bahati mbaya Simba ililazimika kuisubiri pesa hiyo kwa miaka mitatu.. . Tofauti na Okwi, hakuna mchezaji mwingine kutoka Ligi ya Tanzania amewahi kuuzwa zaidi ya Milioni 300.. Hivyo ofa ya Miquissone ni rekodi mpya kwa soka letu.. . Hata hivyo inadaiwa kuwa Simba bado haijawa tayari kumuuza Miquissone.. Wanadai kuwa malengo yao Afrika ni makubwa hivyo wanadhani si muda sahihi kumuuza nyota wao.. . Lakini kwa mtazamo wangu Simba ingekubali tu kumuuza Miquissone.. Kuna faida nyingi katika biashara hiyo. . Kwanza katika biashara hiyo, Simba itapiga pesa.. Usajili wa Miquissone haukugharimu zaidi ya dola 200,000 lakini leo Simba inamuuza kwa Dola 700,000.. Ni faida kubwa.. . Ni mchezaji gani mwingine Simba inaweza kumuuza kwa faida kubwa hivyo? Hakuna. Siyo Chama wala Bwalya.. . Pili, kwa kumuuza Miquissone kwenda klabu kubwa Afrika itavutia wachezaji wengi zaidi kwenda Simba.. Wataona Simba ni daraja la mafanikio.. . Simba itakuwa na heshima yake kwenye soko la usajili.. Wachezaji wengi wenye ndoto kama za Miquissone watatamani kwenda Simba. Vipi Simba ikigoma kumuuza? Wachezaji wakubwa wataona Simba siyo timu nzuri ya kuwafikisha wanapotaka.. . Asikwambie mtu, hakuna mchezaji yoyote mkubwa Afrika hatamani kucheza Al Ahly, Wydad Club au Mamelodi Sundowns.. Ndio timu za ndoto za wengi..