DILI LA MIQUISSONE LIMEIVA KUELEKEA AL AHALY,BILION 2 AITEMA KAIZER CHIEF by @Dream Online Tv (VENICE MEDIA) - Post Details

DILI LA MIQUISSONE LIMEIVA KUELEKEA AL AHALY,BILION 2 AITEMA KAIZER CHIEF

Kuna faida nyingi Simba ikimuuza Miquissone Al Ahly . . Nimeona mijadala na taarifa nyingi zinaendelea kuhusu Luis Miquissone.. Inasemekana kuna timu nyingi kubwa kutoka nje zinamhitaji.. Inapendeza sana.. . Nasikia kuna ofa inayofikia Bilioni 1.6 imetolewa na Al Ahly ya Misri kwa Miquissone.. Ni pesa nyingi sana.. Inatokea mara chache kwa mchezaji kutoka Ligi ya Tanzania akauzwa pesa nyingi hivyo.. . Ilitokea kwa Okwi miaka mingi nyuma.. Aliuzwa Dola 300,000 (Mil 450 kwa wakati huo)... Bahati mbaya Simba ililazimika kuisubiri pesa hiyo kwa miaka mitatu.. . Tofauti na Okwi, hakuna mchezaji mwingine kutoka Ligi ya Tanzania amewahi kuuzwa zaidi ya Milioni 300.. Hivyo ofa ya Miquissone ni rekodi mpya kwa soka letu.. . Hata hivyo inadaiwa kuwa Simba bado haijawa tayari kumuuza Miquissone.. Wanadai kuwa malengo yao Afrika ni makubwa hivyo wanadhani si muda sahihi kumuuza nyota wao.. . Lakini kwa mtazamo wangu Simba ingekubali tu kumuuza Miquissone.. Kuna faida nyingi katika biashara hiyo. . Kwanza katika biashara hiyo, Simba itapiga pesa.. Usajili wa Miquissone haukugharimu zaidi ya dola 200,000 lakini leo Simba inamuuza kwa Dola 700,000.. Ni faida kubwa.. . Ni mchezaji gani mwingine Simba inaweza kumuuza kwa faida kubwa hivyo? Hakuna. Siyo Chama wala Bwalya.. . Pili, kwa kumuuza Miquissone kwenda klabu kubwa Afrika itavutia wachezaji wengi zaidi kwenda Simba.. Wataona Simba ni daraja la mafanikio.. . Simba itakuwa na heshima yake kwenye soko la usajili.. Wachezaji wengi wenye ndoto kama za Miquissone watatamani kwenda Simba. Vipi Simba ikigoma kumuuza? Wachezaji wakubwa wataona Simba siyo timu nzuri ya kuwafikisha wanapotaka.. . Asikwambie mtu, hakuna mchezaji yoyote mkubwa Afrika hatamani kucheza Al Ahly, Wydad Club au Mamelodi Sundowns.. Ndio timu za ndoto za wengi..

Similar Posts!

KOCHA WA ZAMANI SIMBA AFUNGUKA SABABU YA DODOMA JIJI KUFUNGWA NA SIMBA 2-0 KWA MKAPA

FT: Simba 2-0 Dodoma Jijj 🔊 Alama tatu muhimu kwa Simba, Dodoma Jiji wamepoteza mechi ambayo naona walicheza vizuri, walikuwa na nidhamu nzuri ya kuzuia kwa bahati mbaya kosa moja kubwa likawafanya waikabidhi mechi mikononi mwa Simba. 🔊 Dodoma Jiji hawakuwaruhusu Simba kupiga penetration passes, walizuia half spaces na kuwafanya wacheze nje ya eneo la hatari muda mwingi, katika system ya low blocks defensive hukuona Simba wanatengenezaje nafasi kabla ya kosa la penati kutokea. 🔊 Ipo sehemu ya Simba kujitazama mara mbili, mara nyingi wanapokutana na timu za aina hii wanajenga mashambulizi yao taratibu hiyo inawasaidia wapinzani kujipanga kwa sababu presha inakuwa ni ndogo kwenye eneo lao. 🔊 Zipo nyakati ambazo Dodoma Jiji wangekuwa wakatili mbele ya lango la Simba pengine wangeifanya mechi kuwa ngumu zaidi, ni rahisi kukishinda kiungo cha Simba kama utaamua kuwa press na kufanya mikimbio nyuma ya safu hiyo. 🔊 Viungo wa Simba wanapitika kirahisi timu isipokuwa na mpira, tofauti ilikuwa ndogo tu, Dodoma Jiji hawakuwa na ubora katika kufanya matendo ya mwisho ya kutengeneza nafasi na kufunga magoli na hii inaficha udhaifu wa wapinzani ulioonekana

ONA ALICHOKISEMA SHABIKI WA SIMBA ANAEMKUBALI FISTON MAYELE BAADA YA SIMBA KUWAFUNGA DODOMA JIJI

✍Simba SC hawakuwa katika ubora ambao wenyewe wangetamani lakini wamevuna alama 3 , katika mechi zote za msimu ngumu mechi zote ucheze kwa kiwango cha juu , muhimu ni kukusanya alama tatu ndio waliciofanya leo dhidi ya Dodoma FC ambao hawakuonesha madhara kwenda mbele . ✍Dodoma FC dakika kama 5 au 10 za mwanzo walianza na BACK 3 lakini wakaibadilisha haraka na kwenda 4-3-3 wakiwa na mpira na 4-4-2 bila mpira , hawakutaka kuzidiwa idadi ya wachezaji katikati ya uwanja na pembeni ya uwanja... lakini bado mara kadhaa waliacha spaces kubwa sana baina ya mstari mmoja na mwingine na mchezaji kwa mchezaji ✍Ni Simba tu wenyewe , Dodoma ni kama vile hawakuwa na mpango au maono ya kutafuta goli, walikuwa tayari kufungwa ( Dodoma was there for taking ) ...Simba hasa kipindi cha kwanza walikuwa slow sana , umakini unakosekana , walikuwa wanacheza kama wanaongoza 3 au 4 , mpira haukutembea kwa haraka kutoka sehemu moja kwenda nyingine ...viungo watatu ( Chama Nyoni Mzamiru ) + mawinga wawili ( Banda na Sakho ) wote wanacheza mbele ya Dodoma ...hakukuwa na mikimbio ya kutosha nyuma ya kiungo cha Dodoma na safu ya ulinzi ya Dodoma ( Easy to defend ) ✍Nafikiri Dodoma walicheza bila imani kwamba wanaweza kufunga au kupata chochote kitu dhidi ya Simba ,kuna muda walikuwa " Casual " sana , jinsi idadi ya mipira waliyokuwa wanapoteza kirahisi , iwe kwenye kiungo mpaka pembeni ya uwanja ( Sloppy ) nafikiri hata Wawa na Onyango wanaweza wakaangaliana na kujiuliza " Hivi leo mbona hatuna kitu cha kuzuia ? " 😀 NOTE 1: George Wawa sijui alikuwa anafikiria nini ? Alijua refa hatomuona kushika mpira kwa staili ile ? Doh 😀😀 na bado akabisha,Chama Jr alituliza akili licha ya wachezaji wa Dodoma kumfanyia " Mind game" 2: Cleophace Mkandala ..amekosa tu msaada kutoka kwa wenzake,maana ndio mchezaji pekee ambaye akiwa na mpira ndio unaona anaweza kufanya jambo. 3: Positive nyingine kwa Simba ukiacha alama 3 ni kurejea kutoka kwenye majeraha baadhi ya wachezaji 4: Peter Banda hakuacha kujaribu kutengeneza nafasi mpaka akapata assist yake kwa Kagere. Never give up 5: Dodoma inaonekana bado inasukwa ..muda unakimbia FT: Simba 2-0 Dodoma FC

UTACHEKA!! SHABIKI SIMBA ATEMA SHOMBO BAADA YA KUWAFUNGA 2-0 DODOMA JIJI KWA MKAPA