Content removal request!


NDANDA FC 1-0 AZAM FC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 18/04/2019)

Azam FC wamekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Ndanda SC kwenye mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara iliyochezwa leo jioni Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara. Bao pekee la Ndanda limefungwa na Mohamed Mkopi dakika ya 62 akimalizia kwa kichwa mpira wa ‘free-kick’ uliopigwa na Kigi Makasi nje kidogo ya eneo la 18. Ushindi huo wa Ndanda SC dhidi ya Azam FC umeibeba kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya sita ikifikisha pointi 43 huku Azam FC ikiendelea kusalia kwenye nafasi ya pili na pointi zake 66.