Timu ya African Lyon ambayo tayari imeshuka daraja, imejiongezea pointi moja baada ya kutoka sare na Mbeya City, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Lyon ndiyo waliotangulia kupata mabao yote mawili kupitia kwa Musht Bartoz dakika ya 21 na Awadhi Juma dakika ya 45+2 lakini Mbeya City walitumia dakika kumi za mwisho kusawazisha kupitia kwa Victor Hangaya dakika ya 82 na Mohamed Kapeta dakika ya 90+5. Matokeo hayo yameifanya Lyon kufikisha pointi 23 ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi huku Mbeya City ikifikisha pointi 47 na kupanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya saba sawa na Ndanda SC ambayo imeshuka hadi nafasi ya nane.
KARIAKOO DERBY: Yanga SC imeendeleza ubabe kwa kuichapa Simba mabao 2-1 kwa mara ya pili msimu huu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC #NBCPremierLeague uliopigwa leo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Magoli ya Yanga yamefungwa kipindi cha kwanza na Stephane Aziz Ki kwa penati dakika ya 20 na Joseph Guede dakika ya 38.
Kwa TKO raundi ya sita, Mada Maugo amemkalisha Karim Mandonga.
Tazama mikwaju yote ya penati iliyopigwa kwenye mchezo CRDB Bank Federation Cup kati ya Mashujaa FC dhidi ya Simba SC. Simba imetolewa kwa jumla ya penati 6-5 Waliopiga kwa upande wa Simba ni Mohamed Hussein, Israel Mwenda, Freddy Michael Koublan, Willy Onana, Mzamiru Yassin, Ladack Chasambi, Sadio Kanoute Waliopiga kwa upande wa Mashujaa ni Zuberi Dabi, Samson Madeleke, Masinda, Idrissa Stambuli, Adam Adam, Mpoki Mwakinyuke, Baraka Mtui
“Kama klabu lazima tuoneshe kwamba kuna namna ambavyo hatujaridhishwa na kile ambacho kimetokea katika mchezo ule” sehemu ya maneno ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe akizungumzia hatua ambazo timu hiyo imepanga kuzichukua juu ya yale yaliyojiri katika dimba la Loftus kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Tazama taarifa mbalimbali za maandalizi ya Simba na Yanga SC kuelekea mechi zao za marudiano za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika.
Tazama kipindi cha Mshikemshike Viwanjani ambacho kimekusanya habari mbalimbali ikiwemo taarifa ya Rais wa Yanga, Hersi Said akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo. Mashabiki wa Yanga wameanza safari ya kwenda Mamelodi
DAR DERBY: Yanga SC imeangukia pua kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC, katika #DarDerby iliyopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Yanga imetangulia kupata bao kupitia kwa Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Azam kuchomoa dakika ya 19 kwa goli la Gibril Sillah na kisha Feisal Salum akafunga la ushindi dakika ya 51.
DAR DERBY: Yanga SC imeangukia pua kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC, katika #DarDerby iliyopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Yanga imetangulia kupata bao kupitia kwa Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Azam kuchomoa dakika ya 19 kwa goli la Gibril Sillah na kisha Feisal Salum akafunga la ushindi dakika ya 51.