Alichosema Kocha wa Simba Baada Ya Ushindi na Nkana
Alichosema Kocha wa Simba Baada Ya Ushindi na Nkana

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza kuwania kufunzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Nkana FC ya Zambia imemalizika kwa Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Dakika 5 za mwanzo Simba walianza vizuri ila ndani ya dakika 15 walipoteana na kuruhusu bao la dakika ya 16 lililofungwa na Walter Bwalya baada ya kushambulia lango la Simba kwa muda mrefu. Iliwalazimu Simba wasubiri mpaka dakika ya 29 akimalizia pasi ya Claytous Chama na dakika ya 45 Meddie Kagere aliandika bao kwa kichwa akimalizia pasi ya James Kotei. Kipindi cha pili dakika ya 88 Claytous Chama alifunga bao akimalizia pasi ya Hassan Dilunga. Simba wanafanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3 Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars/ Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars/ Twitter: https://twitter.com/kidanistars



MAGOLI YANGA  VS MBAO FC 2-0
MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0

#YANGAvsMBAO MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0 Yanga imefanikiwa kuapata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Taifa Dar es salaam. Bao la kwanza limepachikwa kimiani na Rafel Daud mnamo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kwa njia ya kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajibu. Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, kipindi cha pili Mbao walijitahada kuja kwa kasi kushambulia lango la Yanga lakini haikuweza kusaidia kitu. Licha ya mashambulizi hayo, Mbao FC walipata nafasi zingine kama nne kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia vema. Zikiwa zimeongezwa dakika tano, Ibrahim Ajibu alifanikiwa kuingia kambani kwa kufunga bonge la bao kwa tikitaka ya aina yake na kuifanya Yanga iwe mbele kwa mabao 2-0. Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 2 na Mbao FC 0. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 16 katika msimamo wa ligi huku Mbao ikisalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya 5. GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOKInstall



GOLI la Makambo Yanga VS Coastal Union 1 -0
GOLI la Makambo Yanga VS Coastal Union 1 -0

#MAKAMBO #YANGA GOLI la Makambo Yanga VS Coastal Union 1 -0 Timu ya Yanga imeendelea kujiwekea malengo mazuri ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union. Mchezo huo ulioshuhudiwa ukipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ulizitikisa nyavu za wagosi wa kaya mnamo dakika ya 12 kupitia kwa Heritier Makambo 'Makambovic'. Bai hilo limeisaidia Yanga kujikusanyia jumla ya alama 9 mpaka sasa ikishinda mechi zake zote tatu. Katika mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alimuanzisha kama kawaida kipa mkongomani Klaus Kindoki ambaye alipokea lawama kali katika mechi iliyopita. Kindoki aliruhusu kufungwa mabao matatu matatu dhidi ya Stand United huku wakiibuka na ushindi wa mabao 4-3 lakini leo ameonekana kulitendea haki lango la timu yake. http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://ww.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Suazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli.. Category



HIGHLIGHTS: NDANDA FC 0-0 SIMBA SC (TPL - 15/09/2018)
HIGHLIGHTS: NDANDA FC 0-0 SIMBA SC (TPL - 15/09/2018)

‘Wana-kuchele’ Ndanda SC leo wamevunja mwiko wa kutopata ushindi mbele ya Mnyama mkali Simba baada ya kuilazimisha suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara. Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja, wenyeji Ndanda waliingia na mbinu ya kuzuia zaidi na kuwaacha Simba wacheze mpira hasa kwenye eneo ambalo halikuwa na hatari yoyote. Mabingwa watetezi, Simba licha ya kuwaanzisha washambuliaji watatu machachari, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco, ilishindwa kutengeza nafasi za wazi kutokana na washambuliaji hao kudhibitiwa vilivyo na mabeki wa Ndanda. Hadi mwisho wa mchezo, Simba ilikuwa imepiga jumla ya mashuti 17 ambapo kati ya hayo ni mashuti matatu pekee ndiyo yaliyolenga lango, huku Ndanda wakiwa wamepiga jumla ya mashuti matatu na moja pekee likiwa ndilo limenga lango. Hii ni mara ya kwanza Ndanda FC inakataa kufungwa na Simba, tangu ipande Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2013. Baada ya mchezo huo, Nahodha wa Simba John Bocco amesema licha ya matokeo hayo kutowafurahisha, wanayasahau na kuanza kujipanga kwaajili ya mchezo ulio mbele yao huku kocha wa Ndanda Malale Hamsini akisema aliamua kutumia mbinu hiyo kutokana na ukubwa wa timu ya Simba. Matokeo hayo yanaiweka Simba katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7, huku Ndanda wakifikisha pointi 4 katika nafasi ya 12.



SINGIDA UNITED 3-2 MAJIMAJI FC; MAGOLI YOTE (VPL - 19/05/2018)
SINGIDA UNITED 3-2 MAJIMAJI FC; MAGOLI YOTE (VPL - 19/05/2018)

Timu ya Singida United imefanikiwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Majimaji FC ya Mjini Songea. Singida United walifanikiwa kufunga mabao matatu kupitia kwa Deus Kaseke, Shafiq Batambuze na Tafazwa Kutinyu hadi kipindi cha kwanza cha mchezo. Kipindi cha pili Majimaji walibadilika na kuanza kushambulia lango la Singida United na kufanikiwa kufunga magoli mawili ambayo hayakuwa na msaada kwa upande wao kufuatia kupoteza mchezo kwa mabao 3-2. Tazama hapa mabao yote matano.



SINGIDA UNITED 0-1 SIMBA SC;  HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (VPL 12/05/2018)
SINGIDA UNITED 0-1 SIMBA SC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (VPL 12/05/2018)

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, wameendeleza moto wao kwenye ligi hiyo msimu huu kwa kuichapa Singida United bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya 28 uliopigwa kwenye dimba la Namfua, mjini Singida. Katika mchezo huo ambao Singida United walicheza vizuri zaidi kwa kumiliki mpira kwa asilimia 61 dhidi ya asilimia 39 za Simba, mabingwa hao walipata bao lao pekee kupitia kwa Shomari Kapombe aliyetumia vyema makosa ya walinzi wa Singida United. Bao hilo ndilo lilikuwa shuti pekee la Simba kwenye mchezo huo lililolenga lango, wakiwa pia wamepiga mashuti mawili pekee ambayo hayakulenga lango kwa dakika zote 90, huku Singida United wkipoteza nafasi lukuki za kufunga.



KOCHA AZAM FC: SIMBA HAWANA LOLOTE, WAMEBAHATISHA
KOCHA AZAM FC: SIMBA HAWANA LOLOTE, WAMEBAHATISHA

KOCHA AZAM FC: SIMBA HAWANA LOLOTE, WAMEBAHATISHA SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi. Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..



KOCHA SIMBA Afungukia Siri ya Ushindi Dhidi ya Azam
KOCHA SIMBA Afungukia Siri ya Ushindi Dhidi ya Azam

KOCHA SIMBA Afungukia Siri ya Ushindi Dhidi ya Azam SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi. Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..




« Previous Next »


Popular Tags

#Best Goalkeeper Saves  #James Harden  #Goalkeeper Saves  #Chris Paul  #Golden State Warriors  #Kevin Durant  #David Silva  #Counter Attack Goals Football  #Thomas Muller  #Derrick Rose  

Popular Users

#katzm  #DjokerNole  #AntDavis23  #Buster_ESPN  #billbarnwell  #RealSkipBayless  #BMcCarthy32  #katyperry  #DeionSanders  #BeingSalmanKhan  #Drake  #SportsCenter  #DanicaPatrick  #TimTebow