GOLI LA OKWI SIMBA 1-0 AZAM
GOLI LA OKWI SIMBA 1-0 AZAM

Please watch: "MAGOLI YOTE YA SIMBA 5 - 0 MBAO" https://www.youtube.com/watch?v=lU7L3hP4BP0 --~-- SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi. Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. Dalili za Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma kupata bao zilionekana mapema tu mchezo huo ulipoanza kutokana na mashambulizi yake mfululizo langoni mwa wapinzani. Azam FC walizidiwa katika safu ya kiungo na kujikuta wanawapa fursa Simba kutawala mchezo sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza. Benchi la Ufundi la Azam chini ya Mromania, Aristica Cioaba ba mzalendo, Iddi Cheche liliona hilo na mapema kipindi cha pili wakamuingiza kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Iddi Kipagwile. Mabadiliko hayo yaliipa uhai Azam FC na kuanza kupeleka mashambulizi makali langoni mwa Simba, lakini kipa namba moja nchini, Aishi Manula alisimama imara kuokoa akisaidiwa na mabeki, Yussuph Mlipili na Erasto Nyoni. Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Yussuph Mlipili, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk59, John Bocco, Emmanuel Okwi/Nicholaus Gyan dk84 na James Kotei. Azam FC; Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Iddi Kipagwile/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk55, Frank Domayo, Mbaraka Yussuph, Yahya Zayed/Bernard Arthur dk71 na Enock Atta-Agyei.



MAKOCHA WATIA NENO, SIMBA ILIVYOICHARAZA MAJIMAJI NNE BIILA
MAKOCHA WATIA NENO, SIMBA ILIVYOICHARAZA MAJIMAJI NNE BIILA

Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Jumapili. Mabao ya Simba yalifungwa na washambuliaji John Bocco (2) na Emmanuel Okwi (2), Majimaji walifanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Simba lakini hayakuzaa matunda



HIGHLIGHTS  YANGA VS  MTIBWA SUGAR
HIGHLIGHTS YANGA VS MTIBWA SUGAR

Katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom, ambapo Yanga ilicheza dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo had mwisho wa mchezo matokeo yalibaki bila bila, tumekuwekea kosa kosa za time zote mbili na mashambulizi Katika kila lango. SUBSCRIBE YOUTUBE CHANEL YETU: https://www.youtube.com/channel/UC5fu... https://www.youtube.com/channel/UC5fu... https://www.youtube.com/channel/UC5fu... https://www.youtube.com/channel/UC5fu... https://www.youtube.com/channel/UC5fu... WEBSITE: http://shutikali.co.tz/ http://shutikali.co.tz/ http://shutikali.co.tz/ http://shutikali.co.tz/ http://shutikali.co.tz/ http://shutikali.co.tz/ http://shutikali.co.tz/ http://shutikali.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/shutikali/ https://www.facebook.com/shutikali/ https://www.facebook.com/shutikali/ INSTAGRAM: https://www.instagram.com/shutikali_tz




« Previous


Popular Tags

#Gareth Bale  #Kawhi Leonard  #Counter Attack Goals Football  #Michael Jordan  #Tristan Thompson  #Manuel Neuer  #Paul George  #Paul Pogba  #Luis Suarez  #Shaquille O'Neal  

Popular Users

#RyanBabel  #BMcCarthy32  #TheRealJRSmith  #serenawilliams  #DeionSanders  #mcuban  #AdamSchefter  #justinbieber  #TheCUTCH22  #imVkohli  #oldhossradbourn  #SimplyAJ10  #floydmayweather  #KDTrey5  #ArianaGrande