Baada ya Simba kupoteza point mbili Shinyanga kwa kutoka sare dhidi ya Mwadui FC, leo walionekana kufuta makosa na kuifunga Mbao FC magoli 5-0, magoli ya Simba yakofunhwa ma Shiza Kichuya dakika ya 38, Okwi aliyefunga mawili dakika ya 41 kwa penati na 68, Erasto Nyoni dakika ya 82 na Nikolaos Gyan dakika ya 86.
Magoli yote ya Simba Sc dhidi ya Mbao Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara..Magoli ya Simba yamefungwa na Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi (2), Erasto Nyoni na Nicholas Gyan.
Simba imeicharaza Mbao FC jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa leo katika dimba la Taifa Dar es Salaam. Magoli yote a Simba katika mchezo wa leo, haya hapa, wafungaji wakiwa ni Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi mabao mawili, Nicholas Gyan na Erasto Nyoni.
Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaopigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam.
Please watch: "MAGOLI YOTE YA SIMBA 5 - 0 MBAO" https://www.youtube.com/watch?v=lU7L3hP4BP0 --~-- SIMBA SC imezidi kuwaacha mbali wapinzani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hongera kwake mfungaji wa bao pekee la leo, mshambuliaji Mganda Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga dakika ya 36 baada ya kutokea patashika kwenye lango la Azam FC kufuatia krosi ya beki Mghana, Asante Kwasi. Simba SC sasa inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 17, wakiwazidi kwa pointi saba, mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 34 katika nafasi ya pili na Azam FC wanabaki nafasi ya tatu kwa pointi zao 33. Dalili za Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma kupata bao zilionekana mapema tu mchezo huo ulipoanza kutokana na mashambulizi yake mfululizo langoni mwa wapinzani. Azam FC walizidiwa katika safu ya kiungo na kujikuta wanawapa fursa Simba kutawala mchezo sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza. Benchi la Ufundi la Azam chini ya Mromania, Aristica Cioaba ba mzalendo, Iddi Cheche liliona hilo na mapema kipindi cha pili wakamuingiza kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji Iddi Kipagwile. Mabadiliko hayo yaliipa uhai Azam FC na kuanza kupeleka mashambulizi makali langoni mwa Simba, lakini kipa namba moja nchini, Aishi Manula alisimama imara kuokoa akisaidiwa na mabeki, Yussuph Mlipili na Erasto Nyoni. Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Yussuph Mlipili, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk59, John Bocco, Emmanuel Okwi/Nicholaus Gyan dk84 na James Kotei. Azam FC; Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Iddi Kipagwile/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk55, Frank Domayo, Mbaraka Yussuph, Yahya Zayed/Bernard Arthur dk71 na Enock Atta-Agyei.
Please watch: "MAGOLI YOTE YA SIMBA 5 - 0 MBAO" https://www.youtube.com/watch?v=lU7L3hP4BP0 --~-- Kutoka uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, wekundu wa Msimbazi, Simba Sc imeendelea kutopoteza mchezo wowote katika ligi kuu ya Vodacom baada ya kuzamisha MajiMaji fc ya Songea kwa magoli 4-0. Magoli ya Simba yakifungwa na John Bocco, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya. Endelea kufuatilia ShutikaliTv usipitwe na habari mpya za michezo kila zinapojiri. https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber https://www.youtube.com/channel/UC5fuHg4PI1GAn_U4S5cAOjQ?view_as=subscriber
Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC imeinyanyasa Singida United kwa kuipiga mabao 4-0 katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye dimba la Taifa Dar es Salaam. Mabao ya Simba yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya tatu, Asante Kwasi dakika ya 23 na Emmanuel Okwi aliyetokea benchi dakika ya 65 na kufunga mabao mawili dakika ya 76 na 82.
Please watch: "MAGOLI YOTE YA SIMBA 5 - 0 MBAO" https://www.youtube.com/watch?v=lU7L3hP4BP0 --~-- MSHAMBULIAJI Mganda Emmanuel Arnord Okwi ametokea benchi na kufunga mabao mawili Simba SC ikishinda 4-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matokeo hayo yanaifanya Simba SC ifikishe pointi 29, baada ya kucheza mechi 13, ikiwazidi pointi saba mabingwa watetezi, Yanga SC na pointi mbili Azam FC wenye 27 katika nafasi ya pili, wakati Mtibwa Sugar sasa ni ya tatu kwa pointi zae 24 baada ya timu zote kucheza mechi 13. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, aliyesaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Gasper Ketto wa Arusha hadi mapumziko Simba SC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0. Kiungo Shiza Ramadhani Kichuya alianza kuifungia Simba SC dakika ya tatu akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto, kufuatia John Raphael Bocco kuangushwa nje kidogo ya boksi. Singida wakacharuka na kuanza kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba kusaka bao la kusawazisha, lakini ngome ya Wekundu wa Msimbazi ikiongozwa na Erasto Edward Nyoni ilikuwa imara kuondosha hatari zote. Beki Mghana, Asante Kwasi akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 25 akimvisha kanzu kipa Peter Manyika aliyetoka langoni bila hesabu nzuri baada ya pasi ndefu ya kiungo Said Ndemla aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Kazimoto. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Singida United wanaofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm na kuwaruhusu Simba kutawala zaidi mchezo huo. Kipindi cha pili, mashabiki wa Simba SC wakaripuka kwa shangwe baada ya kumuona kocha wao mpya, Mfaransa Pierre Lechantre aliyeongozana na msaidizi wakea, kocha wa viungo, Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi jukwaa kuu. Kocha huyo amekuja kusaini mkataba wa kuifundisha Simba kuchukua nafasi ya Mcameroon, Joseph Marius Omog aliyeondolewa Desemba na atafanya kazi na Mrundi, Masudi Juma ambaye amekuwa akiiongoza tangu kipindi chote hiki. Okwi akatokea benchi dakika ya 65 kuchukua nafasi ya kiungo Muzamil Yassin na akafunga mabao mawili ndani ya dakika saba. Alifunga bao la tatu dakika ya 75 akimalizia pasi ya Shiza Kichuya na la nne dakika ya 82 akimalizia pasi ya Ndemla. Alifunga mabao hayo, baada ya kumsetia pasi nzuri Kichuya, akapiga nje akiwa ndani ya sita. Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei/Mohammed Ibrahim dk88, Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla dk22, John Bocco, Shiza Kichuyana Muzamil Yassin/Emmanuel Okwi dk65. Singida United; Peter Manyika, Michael Rusheshangoga, Shafiq Batambuze, Kennedy Wilson, Malik Antiri, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Tafadzwa Kutinyu/Yussuf Kagoma79, Lubinda Mundia/Kenny Ally76, Kambale Salita Gentil na Kiggi Makassy/Salum Chukwu dk62.