Stephane Aziz Ki ametoa 'assist' tatu na kufunga goli moja, Yanga ikiichakaza Ihefu kwa kichapo cha mabao 5-0, mchezo wa ligi kuu ya NBC #NBCPremierLeague kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Aliyefungua Dimba alikuwa ni Pacome Zouzoua dakika ya 10, Mudathir Yahya dakika ya 30, Aziz Ki dakika ya 68, Augustine Okrah dakika ya 84 na Maxi Nzengeli dakika ya 86.
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya Azam Sports Federation Cup kati ya Simba SC dhidi ya TRA Kilimanjaro. Magoli matatu yamefungwa na Sadio Kanoute, wengine ni Pa Omar Jobe, Fredy Michael Koublan na Ladack Chasambi
Tazama magoli ya Yanga SC ikiichapa Polisi Tanzania magoli 5-0. Mchezo wa raundi ya tatu ya michuano ya Azam Sports Federation Cup. Magoli yamefungwa na Joseph Guede, Farid Mussa, Clement Mzize na Shekhan Ibrahim
Tazama mambo yalivyokuwa kwenye mechi kati ya JKT Tanzania dhidi ya Simba SC. Goli pekee lililopatikana kwenye mchezo huo limefungwa na Clatous Chota Chama
Clatous Chama ameifungia Simba goli la kusawazisha dakika ya 90 na kufanya matokeo yawe ni sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba, Mwanza. Katika mchezo huo mkali, Azam walitangulia kwa goli la Prince Dube dakika ya 14.
Simba SC imepata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Magoli ya Simba yametoka kwa Pa Omar Jobe, Sadio Kanoute, Che Malone Fondoh na Fredy Koublan.
Goli pekee la njia ya penati kutoka wa Saidi Ntibazonkiza limeipa Simba pointi tatu muhimu, kwa kuichapa Mashujaa FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Tazama highlights.....
Yanga SC imebanwa mbavu na kulazimishwa suluhu na Kagera Sugar kwenye Dimba la Kaitaba, Bukoba, mchezo wa ligi kuu ya NBC #NBCPremierLeague Tazama baadhi ya matukio muhimu kutoka kwenye mchezo huo....