Magoli manne yamefungwa, Yanga ikishinda 4-0 ugenini dhidi ya Vital'o ya Burundi, mchezo wa kwanza hatua ya awali kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika ukipigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Wafungani ni Prince Dube dakika 6, Clatous Chama dakika ya 68, Clement Mzize dakika ya 74 na Stephane Aziz Ki kwa penati dakika ya 90.
Magoli matano yamefungwa, Yanga ikishinda 4-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa fainali #NgaoYaJamii2024 ikipigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar s Salaam. Magoli ya Yanga yametoka kwa Prince Dube 19', Yoro Diaby 28' goli la kujifunga, Stephane Aziz Ki 31' na Clement Mzize 90’+3 , huku Azam FC wakitangulia kwa goli la Feisal Salum Feitoto 13'.
KARIAKOO DERBY | Goli pekee kutoka kwa Maxi Nzengeli dakika ya 44 limewapeleka Yanga fainali ya #NgaoYajamii2024 wakiwafunbga Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa Dimba la Benjamin Mpaka, Dar es Salaam
Debora Fernandes na Edwin Balua ndiyo waliotikisa nyavu, Simba ikiitandika APR FC ya Rwanda magoli 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kuhitimisha sherehe za kilele cha #SimbaDay2024 ndani ya Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
#ToyotaCup: “…..kila kombe ni muhimu” – Clatous Chama kuhusu mchezo wa leo, azungumzia hali ya hewa, awakaribisha wananchi kwenye kilele cha Siku ya Mwananchi. FT: Kaizer Chiefs 0-4 Yanga SC (Dube 25’, Aziz Ki 45’+3, 63’, Mzize 57’) Ilikuwa LIVE #AzamSports1HD #ToyotaCup2024 #YangaSC #KaizerChiefs
#MpumalangaPremiersInternationalCup2024: “Kuna watu walikuwa na shidashida kidogo za ndoa, matatizo yameanza kupungua” maneo ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe akizungumzia namna mechi yao ya leo dhidi ya Augsburg ilivyoleta neema kwa baadhi ya watu. Ametolea ufafanuzi kuhusu ushiriki wao kwenye michauno ya #MpumalangaPremiersInternationalCup2024 Matokeo ni FC Augsburg 2-1 Yanga SC #MpumalangaPremiersInternationalCup2024 #Mpumalanga #YangaSC #FCAugsburg #AUGYNG
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Crescentus Magori na Meneja wa Habari wa timu hiyo Ahmed Ally wamezungumzia mchakato wa usajili ndani ya klabu hiyo na kutoa tafsiri ya ubwaya ubwela.
“Unaweza kumuacha Chama halafu baadaye ukaanza kujuta” – Ahmed Ally kuhusu ishu ya kiungo wao Clatous Chama akifafanua sababu za kuchelewa kufanya maamuzi, asema hatma yake wanayo viongozi wa juu…. asisitiza “yule siyo mtu mchezaji wa kawaida”