YANGA SC 3-1 MWADUI FC HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL-15/1/2019)
YANGA SC 3-1 MWADUI FC HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL-15/1/2019)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC wameendeleza ubabe wao kwenye ligi hiyo msimu huu baada ya leo kuiadhibu Mwadui Fc kwa kipigo cha mabao 3-1, mchezo ukipigwa kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Ajibu kwa ‘free-kick’ dakika ya 12, Amissi Tambwe dakika ya 39 akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu na Feisal Salum kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 58 huku bao la kufutia machozi la Mwadui likifungwa na Salim Aiyee dakika ya 82. Mbali na kupatikana kwa mabao hayo, Ibrahim Ajibu alikosa mkwaju wa penati iliyopanguliwa na golikipa wa Mwadui FC Anold Masawe dakika ya 19. Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 53 na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi huku wanaowafuatia Azam Fc wakiwa na pointi 40 na mchezo mmoja mkononi.



MAGOLI YOTE: YANGA SC 3-1 MWADUI FC (TPL – 15/01/2019)
MAGOLI YOTE: YANGA SC 3-1 MWADUI FC (TPL – 15/01/2019)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC wameendeleza ubabe wao kwenye ligi hiyo msimu huu baada ya leo kuiadhibu Mwadui Fc kwa kipigo cha mabao 3-1, mchezo ukipigwa kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Ajibu kwa ‘free-kick’ dakika ya 12, Amissi Tambwe dakika ya 39 akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu na Feisal Salum kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 58 huku bao la kufutia machozi la Mwadui likifungwa na Salim Aiyee dakika ya 82. Mbali na kupatikana kwa mabao hayo, Ibrahim Ajibu alikosa mkwaju wa penati iliyopanguliwa na golikipa wa Mwadui FC Anold Masawe dakika ya 19. Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 53 na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi huku wanaowafuatia Azam Fc wakiwa na pointi 40 na mchezo mmoja mkononi.



AFRICAN LYON 0-1 YANGA SC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 20/12/2018)
AFRICAN LYON 0-1 YANGA SC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 20/12/2018)

Bao pekee kutoka kwa beki Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ limetosha kuipa Yanga pointi tatu mbele ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Ninja amefunga goli hilo kwa kichwa dakika ya 64 akimalizia mpira wa adhabu ndogo ulipigwa na Ibrahim Ajibu, bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo na kuendeleza rekodi ya ushindi na kutopoteza mchezo kwa Yanga tangu kuanza kwa ligi msimu huu. Ushindi huo unaifanya Yanga izidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 47, mbele ya Azam wenye pointi 40 na Simba wenye pointi 30.



TANZANIA PRISONS 1-3 YANGA SC: FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 03/12/2018)
TANZANIA PRISONS 1-3 YANGA SC: FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 03/12/2018)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, leo wamefanya kweli Jijini Mbeya kwa kuichapa Tanzania Prisons jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Wenyeji Tanzania Prisons ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Jumanne Elifadhili, penati ambayo ilizua tafrani na kupelekea wachezaji watatu wa Yanga kupata kadi za njano. Yanga waliingia kivingine kipindi cha pili na kusukuma mashambulizi ya kasi hasa baada ya kuingia wachezaji wapya Matteo Anthony, Thabani Kamusoko na Amissi Tambe na kupata bao la kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Ibrahim Ajibu kwa mkwaju wa penati. SUPER SUB: Amissi Tambwe ameingia dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Juma Abdul, akasababisha penati iliyosababisha bao la kusawazisha, kisha akafunga mengine mawili dakika ya 85 na 90+2. Timu zote zililazimika kucheza pungufu baada ya Tanzania Prisons kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati, hali ikaonekana si shwari tena uwanjani na kupelekea vurugu ambazo zilizaa kadi nyekundu mbili, yaani moja kila upande. Mara baada ya mchezo wachezaji Mrisho Ngasa na Laurian Mpalile wamezungumza na kuomba radhi mashabiki kwa kitendo walichoonesha, huku Kocha Mwinyi Zahera akimwaga machozi.



MAGOLI YOTE: TANZANIA PRISONS 1-3 YANGA SC (TPL - 03/12/2018)
MAGOLI YOTE: TANZANIA PRISONS 1-3 YANGA SC (TPL - 03/12/2018)

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, leo wamefanya kweli Jijini Mbeya kwa kuichapa Tanzania Prisons jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Wenyeji Tanzania Prisons ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Jumanne Elifadhili, penati ambayo ilizua tafrani na kupelekea wachezaji watatu wa Yanga kupata kadi za njano. Yanga waliingia kivingine kipindi cha pili na kusukuma mashambulizi ya kasi hasa baada ya kuingia wachezaji wapya Matteo Anthony, Thabani Kamusoko na Amissi Tambe na kupata bao la kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Ibrahim Ajibu kwa mkwaju wa penati. SUPER SUB: Amissi Tambwe ameingia dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Juma Abdul, akasababisha penati iliyosababisha bao la kusawazisha, kisha akafunga mengine mawili dakika ya 85 na 90+2.



KOCHA Yanga Awalipua Wachezaji/ Amtaja Tambwe, Ajibu
KOCHA Yanga Awalipua Wachezaji/ Amtaja Tambwe, Ajibu

KOCHA Yanga Awalipua Wachezaji/ Amtaja Tambwe, Ajibu Timu ya Yanga imeendeleza moto wake ndani ya Ligi kuu baada ya kufankiwa kushinda mchezo wake wa leo dhidi ya Lipuli uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga wamecheza michezo tisa mpaka sasa wakiwa wameshinda michezo nane na kutoa sare mchezo mmoja tu dhidi ya Simba. Mchezo huo ambao Lipuli walizidiwa maarifa kipindi cha kwanza baada ya kuweza kuruhusu bao la mapema lililofungwa na Herietier Makambo dakika ya tisa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mrisho Ngassa. Ushindi huo unawarejesha nafasi ya pili ambayo ilikuwa imekaliwa na Simba, Yanga wamecheza michez 9 na kujikusanyia pointi 25 huku Simba wakiwa na Pointi 23 na vinara wa ligi Azam wamekusanya pointi 27. SUBSCRIBE: Global TV Online: https://goo.gl/nQY3hy Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho



MAGOLI YANGA  VS MBAO FC 2-0
MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0

#YANGAvsMBAO MAGOLI YANGA VS MBAO FC 2-0 Yanga imefanikiwa kuapata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Taifa Dar es salaam. Bao la kwanza limepachikwa kimiani na Rafel Daud mnamo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kwa njia ya kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajibu. Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, kipindi cha pili Mbao walijitahada kuja kwa kasi kushambulia lango la Yanga lakini haikuweza kusaidia kitu. Licha ya mashambulizi hayo, Mbao FC walipata nafasi zingine kama nne kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia vema. Zikiwa zimeongezwa dakika tano, Ibrahim Ajibu alifanikiwa kuingia kambani kwa kufunga bonge la bao kwa tikitaka ya aina yake na kuifanya Yanga iwe mbele kwa mabao 2-0. Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 2 na Mbao FC 0. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 16 katika msimamo wa ligi huku Mbao ikisalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya 5. GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOKInstall




« Previous Next »


Popular Tags

#Paul George  #Shaquille O'Neal  #Chicago Bulls  #Amazing Solo Goals  #Boston Celtics  #Cristiano Ronaldo  #Mesut Ozil  #Best Football Defending Skills  #Goalkeeper Saves  #Kobe Bryant  

Popular Users

#SHAQ  #rogerfederer  #RobGronkowski  #mcuban  #britneyspears  #kobebryant  #SimplyAJ10  #jadande  #lindseyvonn  #katyperry  #baseballpro  #HEELZiggler  #UKCoachCalipari