Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sports Club, wamezoa alama zote sita jijini Mwanza baada ya leo kuishushia kipigo kizito cha mabao 4-1 Alliance FC katika uwanja wa CCM Kirumba. Ushindi wa Simba, umepatikana ikiwa zimepita siku tatu tu, tangu waifunge Mbao FC, mabao mawili kwa moja kwenye uwanja huo huo wa CCM Kirumba. Waliotikisa vyavu leo kwa Simba ni Jonas Mkude, Medie Kagere, Clatous Chama na Hassan Dilunga, huku Alliance FC wikifunga kupitia kwa Israel Patrick Mwenda. Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa wakati Simba akiwararua Alliance FC. #SimbaSC #AlliancevSimba #LigiKuuTanzania ALLIANCE FC 1-4 SIMBA SC | HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (VPL - 19/01/2020)
VITASA NIGHT: Tazama ndonga za Mandonga kwa raundi nne dhidi ya Michael Williams kutoka Canada. Kuna wakati wamelamba sakafu wote wawili kwa wakati mmoja, sijui ni nani aliyemuangusha mwenzake…!!! Mbwembwe na burudani baada ya kukamilika kwa raundi nne, siyo habari tena…!!! Mshindi ni Karim Mandonga kwa pointi Hii ni Boxing In Paradise inayopigwa Paje, Zanzibar Pambano kuu lilikuwa ni Harry Mkacha kutoka Malawi dhidi ya Mtanzania, Hamis Magazeti
MZIZIMA DERBY | Magoli mawili, moja likiwa ni la kujifunga kupitia kwa Nathan Fasika Idumba na Clatous Chama yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC, katika #MzizimaDerby ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.
YANGA DAY: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga SC dhidi ya Aigles du Congo. Goli la Yanga limefungwa na Peter Shalulile na magoli ya Aigles du Congo yamefungwa na Talasy Tonny. FT: Yanga SC 1-2 Aigles du Congo #YangaDay #YangaSC #MwakaniTena #Wananchi #MechiYaKirafiki #YangaSC #AiglesduCongo
SIMBA DAY: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya kirafiki kati ya Simba SC dhidi ya Kenya Police Goli limefungwa na Elvis Rupia. FT: Simba SC 0-1 Police Kenya #SimbaDay #SimbaSC #Miaka90 #MechiYaKirafiki #SimbaSC #KenyaPolice
SIMBA DAY: Eba hii kali…Semaji Ahmed Ally aingia na simba wawili wa porini…Kila mtu abaki mdomo wazi. Neno moja tu kwa semaji Ni shamrashamra za #SimbaDay #SimbaDay #SimbaSC #Miaka90
Fuatilia uchambuzi na mengi yaliyojiri dimbani baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba vs Yanga uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Ndani ya studio Patrick Nyembera akiwa na wachambuzi Abissay Stephen na Godlisten Maro. Matangazo yako LIVE #AzamSports1HD lakini unaweza pia kuitazama kupitia katika #AzamTVMaxApp ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamtvtz/ ►INSTAGRAM: https://www.instagram.com/azamsports2/ ►TWITTER: https://twitter.com/azamtvtz ►FACEBOOK: http://www.facebook.com/azamtvtz ►WEBSITE: http://www.azamtv.co.tz