IBRA CLASS vs ALAN PINA: Hili hapa pambano zima kati ya Mtanzania Ibrahim Class dhidi ya Allan Pina raia wa Mexico, likimalizika kwa Ibra Class kupata ushindi wa KO raundi ya tisa... pambano likiwa ni la raundi kumi. Ni katika #UsikuWaVitasa #MoBoxing uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
KAMWE AKWEPA KUMZUNGUMZIA AZIZ KI: Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe anasema hakuna timu Afrika ambayo haipendi kuwa na mchezaji mwenye daraja la Stephane Aziz Ki, japo amekwepa kuzungumzia kwa undani tetesi zinazomhusisha kurejea mitaa ya Jangwani. Kamwe pia amesema kuna mchezaji walimpandisha thamani makusudi ili watu walipe hela nyingi. Kamwe amesema hayo leo kwenye mahojiano maalumu kupitia kipndi cha U-LIVE cha @ufmradiotz #YangaSC #Kamwe #UFM #ULIVE
Simba SC imenyakua Kombe la Shirikisho la CRDB Bank kwa kuichapa Azam FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Dimba la Gombani Pemba. Goli pekee la ubingwa limefungwa Yahya Zayd ambaye amejifunga dakika ya 62.
Yanga SC imehitimisha msimu wa Ligi Kuuya NBC 2025/26 kwa kishindo, ikiichapa JKT Tanzania mabao 3-0 kwenye Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo na kutwaa ubingwa wa tano mfululizo. Magoli yamefungwa na Prince Dube, Maxi Nzengeli na Laurindo Dilson Maria Depu.
Allan Okello 'Star Boy', amepiga magoli yote matatu #Hattrick , Yanga ikishinda 3-0 dhidi ya TRA United, mchezo wa raundi ya 29, Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Haya hapa magoli yote.
Yanga SC imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, kwa kuwachapa Azam FC mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar. Magoli ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Abdullah 'Bacca', Laurindo Dilson Depu, na Pacome Zouzoua. Hii ni Ligi Kuu ya NBC, raundi ya 28 (bado mbili tu) Tazama highlights
Yanga SC imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, kwa kuwachapa Azam FC mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar. Magoli ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Abdullah 'Bacca', Laurindo Dilson Depu, na Pacome Zouzoua. Haya hapa magoli yote...
Mnyama Simba ametinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank kwa kuichapa Coastal Union mabao 4-0 katika mchezo mchezo wa nusu fainali uliopigwa kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha. Magoli ya mchezo huu yamefungwa na Libase Gueye, Nickson Kibabage, Rushine de Reuck kwa penati na Clatous Chama.
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Mbeya City ambapo Elie Mpanzu ndio amepeleka alama tatu unyamani. Simba imeshinda kwa goli 1-0 ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya