Stephane Aziz Ki amefunga magoli mawili na kufikisha magoli 17 katika mbio za ufungaji bora, Yanga ikiibugiza Dodoma Jiji mabao 4-0 kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma. Ni mchezo wa #NBCPremierLeague uliofunguliwa na goli la Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Aziz kufunga mawili dakika ya 45+3 kwa penati na dakika ya 51, na kisha Maxi Nzengeli akafunga kazi kwa goli la nne dakika ya 78. Magoli yote manne haya hapa....
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Mbeya City ambapo Elie Mpanzu ndio amepeleka alama tatu unyamani. Simba imeshinda kwa goli 1-0 ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya
#NBCPL: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mechi ya NBC Premier League kati ya Simba SC dhidi ya Pamba Jiji FT: Simba SC 2-1 Pamba Jiji Magoli ya Simba yamefungwa na Elie Mpanzu na Libasse Gueye huku goli la Pamba Jiji likifungwa na Mathew Momanyi. #NBCPL #NBCPremierLeague #LigiKuuTanzania #ImenogaZaidi #SimbaVsPambaJiji #SimbaSC #PambaJiji #SimbaPamba
#NBCPL: Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo wa NBC Premier League kati ya Yanga SC ikiwa ugenini dhidi ya Mashujaa FC. Mechi imepigwa katika dimba la Lake Tanganyika Kigoma. Magoli yamefungwa na Mudathir Yahya na Bakari Mwamnyeto FT: Mashujaa 0-2 Yanga #NBCPL #NBCPremierLeague #LigiKuuTanzania #ImenogaZaidi #MashujaaVsYanga #Mashujaa #YangaSC #MSHYNG
Jean Jaques Ngita na Jephte Kitambala Bola wameipa Azam FC magoli mawili muhimu ugenini wakiondoka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha dhidi ya Fountain Gate FC. Haya hapa magoli yote mawili...
LIGI YA VIJANA U17 | Ni Kariakoo Derby ya vijana, Yanga U17 na Simba U17, mchezo umemalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa TFF, Kigamboni Dar es Salaam. Yanga wametangulia kwa goli la Issa Ramadhan dakika ya 15, na Simba kuchomoa dakika za majeruhi... Tazama highlights
Kiungo Allan Okello amefunga magoli mawili katika ushindi wa 3-1, Yanga dhidi ya Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Aliyeitanguliza Yanga kwenye mchezo huu alikuwa ni Duke Abuya, kabla ya Hassan Kabunda kuchomoa kipindi cha kwanza... na Allan Okello akapiga mawili kipindi cha pili.
Kiungo Allan Okello amefunga magoli mawili katika ushindi wa 3-1, Yanga dhidi ya Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Aliyeitanguliza Yanga kwenye mchezo huu alikuwa ni Duke Abuya, kabla ya Hassan Kabunda kuchomoa kipindi cha kwanza... na Allan Okello akapiga mawili kipindi cha pili. Haya hapa magoli...
Yamefungwa magoli matatu.... chuma mbili zikiwekwa kambani na Allan Okello na goli lingine likifungwa na Mudathir Yahya kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Hii ni Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.