KOCHA SIMBA Atoa Taarifa ya MAJERUHI " LIGI ni VITA, SIMBA TUPO TAYARI" by @Mpera Mpera Tv - Post Details

KOCHA SIMBA Atoa Taarifa ya MAJERUHI " LIGI ni VITA, SIMBA TUPO TAYARI"

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wameambulia ushindi wa kwanza kwa msimu wa 2021/22 baada ya kuanza kwa sare katika mchezo wa kwanza walipocheza dhidi ya Biashara United. Ikiwa Uwanja wa Jamhuri,ilipata ushindi kupitia nyota wao Meddie Kagere ambaye alianzia benchi. Alipachika bao hilo dakika ya 69 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 na lilimshinda kipa wa Dodoma Jiji Hussein Masalanga na kuifanya Simba kusepa na pointi tatu.

Similar Posts!

MORRISON, BANDA Walivyokiwasha MAZOEZI ya SIMBA KUELEKEA KUIVAA JWANENG GALAXY...
MORRISON, BANDA Walivyokiwasha MAZOEZI ya SIMBA KUELEKEA KUIVAA JWANENG GALAXY...

Simba wameendelea na Mazoezi yao kuelekea mchezo wao wa marudiano Dhidi ya Jwaneng galaxy utakaopigwa Jumapili ya Oktoba 24 katika dimba la mkapa Jijini Dar es Salaam.



SIMBA Waja na KAULI MBIU Hii Kuelekea MECHI Dhidi ya Galaxy 'IT IS NOT OVER Kazi Iendelee'
SIMBA Waja na KAULI MBIU Hii Kuelekea MECHI Dhidi ya Galaxy 'IT IS NOT OVER Kazi Iendelee'

Simba wanatarajia kucheza mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Dhidi ya Jwaneng galaxy ya Nchini Botswana Jumapili ya Oktoba 24 katika dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam huku wahamasishaji wake wakijitamba kuelekea mchezo huo..



SIMBA Watua USIKU wa MANANE Baada ya KUWAPIGA JWANENG GALAXY, MORRISON, BOCCO, LWANGA Watua KIBABE
SIMBA Watua USIKU wa MANANE Baada ya KUWAPIGA JWANENG GALAXY, MORRISON, BOCCO, LWANGA Watua KIBABE

Kikosi cha Simba kimewasili Nchini Tanzania usiku mara baada ya kucheza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng galaxy katika Uwanja wa Taifa wa Botswana na kupata ushindi wa mabao 2-0 na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya kuvuka hatua inayofuata.



SHANGWE la TAIFA STARS Baada ya KUPINDUA MEZA Benin kwa Bao la MSUVA, SAMATTA Aongoza WENZAKE...
SHANGWE la TAIFA STARS Baada ya KUPINDUA MEZA Benin kwa Bao la MSUVA, SAMATTA Aongoza WENZAKE...

TIMU ya taifa ya Tanzania leo Oktoba 10 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia. Nahodha Mbwana Samata alishuhudia kijana wake Simon Msuva akipachika bao la ushindi mapema dakika ya 6 na lilidumu mpaka dakika ya 90. Ushindi huo unaifanya Stars kufukisha pointi saba sawa na Benin katika kundi J ikiwa inaongoza kwa wakati huu na itafahamika baada ya mchezo wa Dr Congo wenye pointi 5 ambao watacheza na Madagascar ambayo haijakusanya pointi mpaka wakati huu.



FURAHA ya KOCHA KIM Baada ya TAIFA STARS Kupata USHINDI "TULIWASOMA BENIN" Ataja MBINU Aliyotumia...
FURAHA ya KOCHA KIM Baada ya TAIFA STARS Kupata USHINDI "TULIWASOMA BENIN" Ataja MBINU Aliyotumia...

TIMU ya taifa ya Tanzania leo Oktoba 10 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia. Nahodha Mbwana Samata alishuhudia kijana wake Simon Msuva akipachika bao la ushindi mapema dakika ya 6 na lilidumu mpaka dakika ya 90. Katika mchezo wa leo Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ilicheza kwa utulivu mkubwa na kusaka ushindi wa haraka kipindi cha kwanza na baada ya kupata ushindi kazi ya ulinzi na kushambulia kwa kushtukiza iliendelea. Beki wa Stars, Kennedy Juma ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakitumia nguvu nyingi jambo lililopelekea akaonyeshwa kadi ya njano. Ushindi huo unaifanya Stars kufukisha pointi saba sawa na Benin katika kundi J ikiwa inaongoza kwa wakati huu na itafahamika baada ya mchezo wa Dr Congo wenye pointi 5 ambao watacheza na Madagascar ambayo haijakusanya pointi mpaka wakati huu.



KOCHA BENIN Amtaja SAMATTA Baada ya USHINDI DHIDI YA TANZANIA, Waondoka KIBABE...
KOCHA BENIN Amtaja SAMATTA Baada ya USHINDI DHIDI YA TANZANIA, Waondoka KIBABE...

Ni mchezo wa kwanza Stars kupoteza katika kundi J na wanapoteza pointi tatu mazima ikiwa Uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wake. Kwenye msimamo sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na vinara ni Benin wenye pointi 7.