TIMU ya taifa ya Tanzania leo Oktoba 10 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia. Nahodha Mbwana Samata alishuhudia kijana wake Simon Msuva akipachika bao la ushindi mapema dakika ya 6 na lilidumu mpaka dakika ya 90. Ushindi huo unaifanya Stars kufukisha pointi saba sawa na Benin katika kundi J ikiwa inaongoza kwa wakati huu na itafahamika baada ya mchezo wa Dr Congo wenye pointi 5 ambao watacheza na Madagascar ambayo haijakusanya pointi mpaka wakati huu.