Kikosi cha Simba kimewasili Nchini Tanzania usiku mara baada ya kucheza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng galaxy katika Uwanja wa Taifa wa Botswana na kupata ushindi wa mabao 2-0 na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya kuvuka hatua inayofuata.