Content removal request!


KOCHA SIMBA Atoa Taarifa ya MAJERUHI " LIGI ni VITA, SIMBA TUPO TAYARI"

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wameambulia ushindi wa kwanza kwa msimu wa 2021/22 baada ya kuanza kwa sare katika mchezo wa kwanza walipocheza dhidi ya Biashara United. Ikiwa Uwanja wa Jamhuri,ilipata ushindi kupitia nyota wao Meddie Kagere ambaye alianzia benchi. Alipachika bao hilo dakika ya 69 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 na lilimshinda kipa wa Dodoma Jiji Hussein Masalanga na kuifanya Simba kusepa na pointi tatu.