DROO YA ROBO NA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM SPORTS (ASFC) by @Azam TV - Post Details

DROO YA ROBO NA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM SPORTS (ASFC)

Droo ya hatua ya robo na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports imefanyika leo ndani ya Studio za Azam TV ambapo mabingwa wa zamani wa kombe hilo Yanga SC wamepangwa kukutana na Alliance FC, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Wakati Yanga ikipelekwa Mwanza, mabingwa wengine wa zamani wa michuano Azam FC wamepelekwa mkoani Kagera ambako itakutana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba na KMC itacheza na African Lyon. Kwa upande wa wana fainali wa msimu uliopita timu ya Singida United, wao watasafiri hadi mkoani Iringa kukabiliana na Lipuli FC kwenye hatua hiyo ya robo fainali. Kwa upande wa nusu fainali, ratiba imekaa kama ifuatavyo:- Lipuli/Singida United vs Alliance/Yanga. Kagera Sugar/Azam vs KMC/African Lyon

Similar Posts!

USIKU WA VITASA | Karim Mandoga Vs Mada Maugo (TKO) - 11/04/2024
USIKU WA VITASA | Karim Mandoga Vs Mada Maugo (TKO) - 11/04/2024

Kwa TKO raundi ya sita, Mada Maugo amemkalisha Karim Mandonga.

Mashujaa FC 1-1 (6-5) Simba SC | Penati | CRDB Bank Federation Cup - 09/04/2024
Mashujaa FC 1-1 (6-5) Simba SC | Penati | CRDB Bank Federation Cup - 09/04/2024

Tazama mikwaju yote ya penati iliyopigwa kwenye mchezo CRDB Bank Federation Cup kati ya Mashujaa FC dhidi ya Simba SC. Simba imetolewa kwa jumla ya penati 6-5 Waliopiga kwa upande wa Simba ni Mohamed Hussein, Israel Mwenda, Freddy Michael Koublan, Willy Onana, Mzamiru Yassin, Ladack Chasambi, Sadio Kanoute Waliopiga kwa upande wa Mashujaa ni Zuberi Dabi, Samson Madeleke, Masinda, Idrissa Stambuli, Adam Adam, Mpoki Mwakinyuke, Baraka Mtui

Yanga kupeleka malalamiko CAF yaliyojiri mechi yao na Mamelodi Sundowns
Yanga kupeleka malalamiko CAF yaliyojiri mechi yao na Mamelodi Sundowns

“Kama klabu lazima tuoneshe kwamba kuna namna ambavyo hatujaridhishwa na kile ambacho kimetokea katika mchezo ule” sehemu ya maneno ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe akizungumzia hatua ambazo timu hiyo imepanga kuzichukua juu ya yale yaliyojiri katika dimba la Loftus kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

MSHIKESMSHIKE VIWANJANI - 03/04/2024
MSHIKESMSHIKE VIWANJANI - 03/04/2024

Tazama taarifa mbalimbali za maandalizi ya Simba na Yanga SC kuelekea mechi zao za marudiano za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika.

MSHIKEMSHIKE VIWANJANI 01/04/2024
MSHIKEMSHIKE VIWANJANI 01/04/2024

Tazama kipindi cha Mshikemshike Viwanjani ambacho kimekusanya habari mbalimbali ikiwemo taarifa ya Rais wa Yanga, Hersi Said akizungumzia mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo. Mashabiki wa Yanga wameanza safari ya kwenda Mamelodi

Azam FC 2 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 17/03/2024
Azam FC 2 -1 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 17/03/2024

DAR DERBY: Yanga SC imeangukia pua kwa kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC, katika #DarDerby iliyopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Yanga imetangulia kupata bao kupitia kwa Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Azam kuchomoa dakika ya 19 kwa goli la Gibril Sillah na kisha Feisal Salum akafunga la ushindi dakika ya 51.

Magoli | Azam FC 2-1 Yanga SC | NBC Premier League 17/03/2024

Simba 2-0 Mashujaa | Highlights | NBC Premier League 15/03/2024
Simba 2-0 Mashujaa | Highlights | NBC Premier League 15/03/2024

Clatous Chama amefunga magoli mawili muhimu dakika ya 57 na 73, Simba ikipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mashujaa FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa #AzamComplex, Chamazi .