Simba SC 'yafumua' mfumo wa kikosi ili kuwakabili Mwadui FC hapo kesho kwenye dimba la Kambarage mkoani Shinyanga: Watafuta machungu waliyopewa na Mbao FC? Yanga SC kuendelea za wimbi la ushindi Dar? Azam FC je, suluhu zitaendelea ugenini? Kwa haya na mengine mengi ya kimichezo ungana na Ahmed Abdallah katika MSHIKEMSHIKE VIWANJANI.
Baada ya kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC, mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba SC leo wameendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakisema wamerekebisha mfumo mzima wa kikosi chao ili waweze kushinda dhidi ya Mwadui FC kesho Jumapili Septemba 23, 2018 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Meneja wa timu hiyo Abbas Ally anazungumzia marekebisho hayo.