Azam FC imeitandika Singida Black Stars mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi..... Magoli ya Azam FC yametoka kwa Feisal Salum na Jhonier Blanco huku Singida wakpata bao lao kupitia kwa Elvis Rupia...
Yanga SC imepoteza mchezo wa pili mfululizo kwenye ligi baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo Azam Complex, Chamazi. Offen Chikola amefunga magoli mawili dakika ya 19 na 45 ... huku Nelson Munganga akifunga la tatu dakika ya 78. Goli la kufutia machozi kwa Yanga limefungwa na Clement Mzize dakika ya 90. Yanga pia walipata penati dakika ya 45 ikipigwa na Stephane Aziz ki lakini ikadakwa na golikikpa Hussein Masalanga....
Simba SC imeichakaza KMC mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam..... Magoli ya Simba yamefungwa na Awesu Ally Awesu dakika ya 25, Jean Charles Ahoua mawili dakika ya 38' kwa penati na dakika ya 69', na lingine limetoka kwa Edwin Balua dakika ya 66. Haya hapa magoli yote manne.....
John Bocco amefunga magoli mawili dakika ya 21 na 26, akiiongoza JKT Tanzania kuichapa Tabora United mabao 4-2 ,katika mchezo wa #NBCPremierLeague uliopigwa kwenye Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo. Dar es Salaam. Magoli mengine yametoka kwa Edward Songo dakika ya 58 na Said Ndemla dakika ya 63... huku magoli ya Tabora United yakifungwa na Offen Chikola dakika ya 42 na Yacouba Sogne dakika ya 90. Haya hapa magoli yote sita....
Klabu ya Yanga imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Augsburg katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mbombela, uliopo Mpumangala Afrika Kusini. Mshambuliaji mpya wa Yanga Jean Baleke ameanza vyema baada ya kufunga bao la kufutia machozi kwa timu yake huku Mads Pedersen na Niklas Dorsch wakiifungia Augsburg. FT: FC Augsburg 2-1 Yanga. Video Credit @azamtvtz @fcaugsburg #samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #augsburg #alahlysc #miraj #baleke #chama #aziziki
Taarifa itakayowashusha presha mashabiki wa Yanga ni kwamba hatimaye kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Stephanie Aziz KI, amewasili nchini huku alitolewa Uwanja wa Ndege kininja. Aziz KI, amewasili nchini alfajiri ya leo Julai 10, 2024 akitokea mapumziko nchini kwao kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia lakini akatoka kimkakati uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere terminal 3. Alichofanya Azizi Ki, kwanza akamtanguliza mfanyakazi mmoja wa Uwanja wa Ndege kutangulia mbele na mabegi yake makubwa sita aliyotua nayo. Hatua ya pili ikawa Ofisa mmoja wa Yanga Godlisten Anderson 'Chicharito' aliyekuja kumpokea uwanjani hapo kumpenyezea kofia maarufu kwa jina la kepu, ambayo kiungo huyo ilipomfikia akatoka akiwa ameishusha kijanja mithili ya mtu asiyetaka kujulikana. Hatua ya tatu akatoka akiwa peke yake huku Ofisa huyo wa Yanga akitangulia mbele wakiachana kwa hatua sita na kiungo huyo kisha kupanda kwenye gari moja aina ya Toyota Alphard iliyotoka uwanjani hapo kwa kasi. Hatua ya nne mara baada ya kufika nje ya uwanja wa Ndege kiungo huyo akakuta gari nyingine aina ya Toyota Harrier ikimsubiri kisha kupanda humo huku ile Alphard ikiondoka na mabegi yake pekee. Ujio wa Azizi Ki ambaye ndiye mfungaji Bora wa Ligi msimu uliopita akimaliza na mabao 21 utawashusha presha mashabiki wa Yanga ambao wanadhani anaweza kuondoka. Yanga bado haijatangaza kwamba Azizi Ki ameongeza mkataba lakini Mwananchi linafahamu kwamba kiungo huyo raia wa Burkina Faso bado ataendelea kuitumikia timu hiyo kufuatia kukubaliana na mabosi wa timu hiyo kwamba atasalia. Pia, kupitia mitandao ya kijamii ya Yanga imetangaza kuwa staa huyo atazungumza mchana wa leo. #samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #alahlytv #alahlysc #miraj
Simba imetumia takriban Million 300 kupata saini ya mshambuliaji wa Zamani wa Asante kotoko Steve Dese Mukwala ambae amemaliza msimu wa ligi kuu nchini Ghana akiwa mshambuliaji namba mbili katika mbio za ufungaji bora nchini Ghana akiwa na mabao 14 Dullah Hassan anatupitisha Katika baadhi ya Rekodi za nyota huyu akiwa nchini Uganda pamoja na Ghana Kama unahitaji kuungwa kwenye group la Simba Pro tuma ujumbe kwa namba 0626629644 ili tuweze kukupa utartatibu wa jinsi ya kujiunga
Tazama magoli yote matano na penati aliyokosa Alikiba katika mchezo wa hisani, Team FEIBUI ikiitandika Team SAMAKIBA mabao 3-2 kwenye Dimba la Amaan Complex, Zanzibar. Magoli ya FEIBUI (Fesal Salum Feitoto na Abdulaziz Makame) yamefungwa na Feisal Salum, Ibrahim Ahmada Hilika, na Dismas Novatus huku magoli ya SAMAKIBA (Mbwana Samatta na Alikiba) yakifungwa na Kelvin John 'Mbappe' na Mbwana Samatta. Dakika ya 24, Team SAMAKIBA walipata penati lakini Alikiba alikosa....