Jumatatu, Machi 24, 2025, ni siku ya kihistoria kwa wapenda soka wa Mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla, kwani klabu ya Singida Black Stars inazindua rasmi uwanja wake mpya. Uzinduzi huu ni hatua kubwa kwa klabu hiyo, ambayo imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo ili kuinua kiwango cha soka nchini. Uwanja huo uliopo Mtipa mkoani Singida, umejengwa kwa viwango vya kisasa ukiwa na nyasi bandia kwa kushirikiana na wadhamini wakuu wakiwamo Airtel, Azam, GSM, NBC, SBS, na MO Dewji. Uwanja huu una uwezo wa kuchukua mashabiki 5,000 hadi 7,000 na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa. Sherehe za uzinduzi zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na michezo, huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA. Aidha, viongozi wa TFF nao wanatarajiwa kushiriki. Burudani mbalimbali zimetayarishwa kabla ya mechi kuu, ikiwa ni pamoja na muziki kutoka kwa wasanii maarufu wa Bongo Fleva, michezo ya asili, na maonesho ya utamaduni wa Kisingida. Mashabiki watapata fursa ya kushuhudia historia ikiandikwa kwa mara ya kwanza kwenye uwanja huu mpya. Kilele cha tukio hili kitakuwa ni mchezo wa kirafiki kati ya wenyeji Singida Black Stars na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC utakaochezwa kuanzia saa 10 jioni. Mechi hii inatajwa kuwa ya kuvutia kutokana na nafasi za timu hizi katika msimamo wa ligi, ambapo Yanga wanaongoza kwa pointi 58 huku Singida Black Stars wakiwa nafasi ya nne na pointi 44. Licha ya kuwa mechi ya kirafiki, upinzani baina ya timu hizi mbili umeibua hamasa kubwa kwa mashabiki. Singida Black Stars wanataka kutumia uwanja wao mpya kuonyesha ubabe wao, huku Yanga wakitaka kuendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya wapinzani wao.
Shabiki wa Yanga Aliyezongwa na Mashabiki wa Simba katika Mchezo wa Simba na Azam FC Benjamin Mkapa, Afunguka Mazito, Aeleza kila kitu, Atinga Polisi.
Timu ya taifa ya Zanzibar… #ZanzibarHeroes imeibuka na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025 kwa kuichapa Burkina Faso mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa leo kwenye Dimba Gombani, Pemba. Zanzibar walitangulia kupata bao dakika ya 41 kwa kisigino cha Ibrahim Hamad Hilika, kisha Burkina Faso wakachomo dakika ya 69 kupitia kwa Aboubacar Traore…. Lakini dakika za majeruhi, Hassan Ali Cheda akafunga la pili na la ushindi kwa Zanzibar.
Hakikisha Umesubscribe Chaneli yetu ya #AyomaMedia kwa habari za uhakika Na pia tufuatilie Katika Mitandao ya Kijamii kama Instagram & Facebook na Twitter kama @Ayoma_tv
DJ Sinyorita akiwarusha mashabiki wa Simba SC hapo jana.
JE UNAHITAJI KUTANGAZA BIASHARA NA WISPOTI TV. KARIBU TUKUHUDUMIE KWA GHARAMA NAFUU, WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0743040370 AU TUCHEKI KUPITIA WHATSAPP NAMBA 0758099136.
"Is a life's and sports channel our vision is to develop and deliver world class Broadcast-based on local and international market" #sports #footballclub #zuchu #azamfc #harmonize #harmonize #singidafountaingate #simbanation #footballclub #sports #soccerclub #footballclub #zuchu #azamfc #middlesimba #harmonize #singidafountaingate #zuchu #simbanation #footballclub #sports #azamfc #middlesimba #harmonize #singidafountaingate