Zimepigwa penati tatu, Simba ikiitandika Namungo FC mabao 3-0 kwenye Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Jean Charles Ahoua amefunga penati mbili, huku Lionel Ateba akikosa penati moja iliyookolewa na golikipa wa Namungo, Jonathan Nahimana. Goli la tatu kwa Simba limefungwa na Steven Mukwala dakika za majeruhi... Katika mchezo huu pia, Namungo wamepata pigo baada ya beki wake Derrick Mukombozi kutolewa kwa kadi nyekundu...
Stephane Aziz Ki amefunga #hattrick ... Yanga ikiitandika KMC mabao 6-1 kwenye dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya NBC. Hat-trick ya Aziz Ki imepatikana kwa penati mbili dakika za 18 na 56, huku lingine lingia nyavuni dakika ya 49. Aliyefungua mlango wa magoli ni Prince Dube dakika ya 10... huku Maxi Nzengeli na Israel Mwenda nao wakifunga dakika za majeruhi... Bao la kufutia machozi limetoka kwa Redemtus Mussa dakika ya 51. Haya hapa magoli yote...
KIPA WA KAGERA AFUNGUKA ALICHOMUAMBIA PACOME KABLA YA KUPIGA PENATI, PACOME FUNDI WA MPIRA
Timu ya Yanga Veteran imefanikiwa kuwa mabingwa wa Ngao ya Jamii ya Ligi ya Maveterani Tanzania #TanzaniaVeteranLeague (TVL) baada ya kuichapa Simba Veteran kwa penati 4-2, kufuatia suluhu ndani ya dakika 90. Mechi imepigwa kwenye Dimba la KMC, Mwange Dar es Salaam...