Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga SC umemalizika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Kwa sare hiyo, Yanga SC inajisogeza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutokana na kujiongezea pointi moja na kufikisha 13 baada ya kucheza mechi tano, nne nyingine zote wakishinda. Kwa upande wao, mabingwa watetezi, Simba SC wanafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi sita, wakitoa sare ya pili leo na kufungwa moja, nyingine tatu wakishinda. Lakini Simba SC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na pointi zote kwenye mchezo wa leo, kwani walifanikiwa kuwazidi wapinzani wao muda wote Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars
Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui Fc katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga. Katika mchezo huo, Simba imewaanzisha washambuliaji wake wawili Meddie Kagere aliyefunga bao moja na John Bocco alioyefunga mawili huku Emmanuel Okwi akiwekwa benchi. Baada ya mchezo huo kumalizika, Meneja wa Simba Abbas Ally amefafanua sababu za kocha kufikia uamuzi huo. Naye Kocha wa Mwadui FC Ally Bizimungu amesema kilichosababisha wafungwe na Simba kwenye mchezo huo ni wachezaji wake kukosa uzoefu.
‘Wana-kuchele’ Ndanda SC leo wamevunja mwiko wa kutopata ushindi mbele ya Mnyama mkali Simba baada ya kuilazimisha suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara. Katika mchezo huo uliokuwa wa upande mmoja, wenyeji Ndanda waliingia na mbinu ya kuzuia zaidi na kuwaacha Simba wacheze mpira hasa kwenye eneo ambalo halikuwa na hatari yoyote. Mabingwa watetezi, Simba licha ya kuwaanzisha washambuliaji watatu machachari, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco, ilishindwa kutengeza nafasi za wazi kutokana na washambuliaji hao kudhibitiwa vilivyo na mabeki wa Ndanda. Hadi mwisho wa mchezo, Simba ilikuwa imepiga jumla ya mashuti 17 ambapo kati ya hayo ni mashuti matatu pekee ndiyo yaliyolenga lango, huku Ndanda wakiwa wamepiga jumla ya mashuti matatu na moja pekee likiwa ndilo limenga lango. Hii ni mara ya kwanza Ndanda FC inakataa kufungwa na Simba, tangu ipande Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2013. Baada ya mchezo huo, Nahodha wa Simba John Bocco amesema licha ya matokeo hayo kutowafurahisha, wanayasahau na kuanza kujipanga kwaajili ya mchezo ulio mbele yao huku kocha wa Ndanda Malale Hamsini akisema aliamua kutumia mbinu hiyo kutokana na ukubwa wa timu ya Simba. Matokeo hayo yanaiweka Simba katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7, huku Ndanda wakifikisha pointi 4 katika nafasi ya 12.
Ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) uliopigwa kwenye dimba la Taifa Dar es salaam na Kagera Sugar kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.
Mshambuliaji nyota wa wa Simba , Emmanuel Okwi, akiongea na wanahabari baada ya kufunga bao dhidi ya ndanda FC
SIMBA VS NDANDA 1-0 ,GOLI la Okwi Lililoipa Simba Points Tatu Kikosi cha Simba kimeendelea kuunusa ubingwa wa Ligi Kuu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC. Bao pekee katika mchezo huo limetiwa kimiani na Mshambuliaji wa kimataifa, Mganda, Emmanuel Okwi. Okwi alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa beki wa kulia, Shomari Kapombe. Matokeo hayaifanya Simba ifikishe alama 65 kwenye msimamo wa ligi huku Ndanda FC wakisalia kwenye nafasi 15 wakiwa na alama 23. lnstal GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli..
Simba yazid kupata ushindi na kujiakikishia kupata ubingwa