Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Bara Yanga SC wameendeleza rekodi ya ushindi kwenye Dimba la Taifa Dar es salaam, safari hii wakiichapa Lipuli FC bao 1-0. Bao pekee la yanga limetiwa nyavuni na mshambuliaji wake Heritier makambo dakika ya 10 akimalizia pasi safi ya Mrisho Ngasa baada ya makossa ya beki wa Lipuli.
Ulipigwa mpira mrefu kutoka golini kwa Mwadui, na Charles Ilanfya kumzidi kasi beki wa Simba Pascal Wawa na kuunganisha nyavuni kwa Simba, akiifungia Mwadui bao la kufutia machozi. Ni mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara ukipigwa kwenye dimba la Kambarage mjini Shinyanga leo Septemba 23, 2016. Hiki ndicho kilichotokea..
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ay Yanga imeendelea kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Coastal Union bao 1-0. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 1:00 jioni ulikuwa na mvuto wa aina yake kutokana na viwango bora vilivyooneshwa na timu zote mbili, Yanga ikiwa na nguvu zaidi kipindi cha kwanza, huku Coastal Union wakitawala zaidi kipindi cha pili. Bao la Yanga kwenye mchezo huo limepachikwa kimiani na mshambuliaji wake Heritier Makambo dakika ya 12 ya mchezo akiitumia vyema pasi ya Ibrahim Ajib, bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo. Hata hivyo dakika ya 35 ya mchezo, Makambo aliingia nyavuni tena lakini mwamuzi akaamua kuwa siyo bao kutokana na Papy Tshishimbi ambaye ndiye aliyetoa pasi ya mwisho, kuwa kwenye eneo la kuotea. Baada ya mchezo huo Azam TV imezungumza na Ibrahim Ajib ambaye ameelezea siri ya kiwango chake kuwa juu kwa siku za karibuni kuwa ni kufuata maelekezo ya mwalimu na kumtegemea Mungu, huku akiwataka mashabiki wa Yanga kujiandaa kuchukua kombe la ligi hiyo msimu huu. Naye kiungo wa Coastal Union Mtenje Albano ameelezea sababu za timu yake kuelemewa zaidi kipindi cha kwanza kabla ya kuingia kwake dimbani.
Timu ya Alliance FC ya Jijini Mwanza imebanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na African Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo CCM Kirumba Jijini Mwanza. Mkongwe, Haruna Moshi 'Boban' ndiye aliyetanguliza African Lyon kwa bao la dakika ya 8 kazi nzuri ikifanywa na Victor Da Costa. Baada ya mshambulizi ya muda mrefu hatimaye Michael Chinedu aliyeingia kutoka benchi aliipa kashikashi safu ya ulinzi ya African Lyon na kuisawazishia timu yake ya Alliance FC dakika za nyongeza. Hata hivyo dakika ya 78 ya mchezo, Alliance walikwamisha mpira nyavuni lakini haikuwa bao ikionekana kuwa kuna faulo ilifanyika kabla yay a bao hilo.