Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Jumapili. Mabao ya Simba yalifungwa na washambuliaji John Bocco (2) na Emmanuel Okwi (2), Majimaji walifanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Simba lakini hayakuzaa matunda