#chama #simbasc #udsongo KIUNGO wa Simba raia wa Zambia, Clatous Chama, Jumamosi iliyopita ilikumbana na balaa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo uliofanyika nchini Msumbiji. Katika mchezo huo, Chama anadaiwa kupewa ulinzi mkali na wapinzani ili kuhakikisha hapati nafasi ya kuanzisha mashambulizi kama ambavyo alikuwa akifanya katika michuano hiyo msimu uliopita. Akizungumza na DREAM ONLINE TV mmoja wa wachezaji wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kuwa, kama Chama katika mchezo huo angekuwa sawa basi wangepata ushindi. “Tunamshukuru Mungu tumerudi salama japokuwa hatukupata ushindi lakini kazi ilifanyika, pia wapinzani wetu walijitahidi sana kuzijua mbinu zetu ambazo tumekuwa tukizitumia kupata ushindi. “Katika mchezo huo Chama hakufanikiwa kufanya vizuri kutokana na ulinzi mkubwa aliokuwa amewekewa na wapinzani wetu hao, kwani kila alivyokuwa akishika mpira tayari kuna watu wawili wanamzunguka jambo ambalo lilisababisha asifanye vizuri kama tulivyotarajia. “Hata hivyo ni matumaini yetu ni kuwa kocha atakuwa ameliona hilo na atalifanyia kazi ili katika mchezo wa marudiano tutakaocheza hapa nchini tuweze kupata ushindi,” alisema mchezaji huyo. Alipoulizwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems alisema: “Mchezo huo ulikuwa wa wazi na tulikuwa tukishambuliana kwa zamu na zaidi wapinzani wetu walijitahidi sana kuhakikisha wanadhibiti sehemu yetu ya kiungo ili viungo wetu wasipate nafasi ya kutengeneza nafasi za kufunga, hata hivyo katika mchezo wa marudiano tutahakikisha tunafanya vizuri katika uwanja wetu wa nyumbani.”
IKICHEZA kwa kujiamini na mbinu za hali ya juu, juzi Jumamosi Simba ililazimisha suluhu ugenini dhidi ya wenyeji, UD Songo ya Msumbiji. Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Beira, Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisisitiza kwamba; “Tunakwenda kumaliza kazi Dar.” Simba iliandika rekodi ndani ya msimu mpya baada ya kutoruhusu bao lolote ikianzia mashindano hayo makubwa ugenini. Msimu uliopita kwenye hatua ya awali Simba ilianzia nyumbani dhidi ya Mbabane ikashinda 4-1, ugenini ikashinda mabao 4-0. Baada ya hapo katika mechi zote ilizocheza ugenini ikaruhusu mabao mengi. Katika mchezo wa jana Simba ilionekana kucheza kwa kujiamini huku safu ya ulinzi ikifanya kazi ya ziada. Ndani ya dakika 45 za kwanza Simba ilipiga mashuti matatu ambayo hayakuwa na madhara lakini mengine mawili nusura yawaamshe mashabiki kwani kipa alipangua yakawa kona. Wekundu hao walipata kona nne za haraka huku wakionekana kutawala zaidi eneo la katikati na kuwalazimisha wenyeji kupiga pasi ndefu ambazo hata hivyo walionyesha udhaifu mkubwa kwenye umaliziaji kwani walikuwa wakipaisha au kupiga pasi fyongo ambazo zilikuwa mboga kwa Benno Kakolanya. UD Songo walicheza mpira wa kuvizia kipindi cha pili lakini wakadhibitiwa na Nyoni na Wawa ambao walionekana kujiamini. Shiboub ambaye ni raia wa Sudan katika mechi jana alitawala kiungo na kuziba mianya mingi ya wenyeji kuwafikia mabeki wa Simba. Mkude muda mwingi alikuwa akiinasa mipira, kuidhibiti na kumpa Chama ambaye kazi yake ilikuwa kusambaza tu. Kwa mujibu wa kocha na viongozi wa Simba, uwanja uliochezwa mechi hiyo wa Campo Do Ferroviario Da Beira ulikuwa chakavu sana na haukuruhusu kucheza kiwango chao ingawa suluhu bado inawabeba. Aussems alisisitiza kwamba wana nafasi kubwa ya kushinda Dar es Salaam kwenye mechi ya marudiano na kusonga mbele na hawana wasiwasi. “Ulikuwa mchezo wa wazi, walikuwa wakijaribu kufunga na kwetu ilikuwa hivyo, jambo muhimu hatujaruhusu goli. Mchezo wa marudiano utakaochezwa Dar ni muhimu, kwa ushangiliaji wa mashabiki wetu na uwanja mzuri nafikiri tutafanya vizuri,” alisema Kocha Aussems.
Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hassan Dilunga, amewaomba radhi viongozi na mashabiki wa JKT Tanzania baada ya kuwafunga jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. #Simba #JktTanzania
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars #SIMBASC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa 1-0 JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 72 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya watani wao wa jadi, #YangaSC wenye pointi 77 za mechi 33. Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya sita kati ya saba za nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, kiungo Hassan Dilunga aliyetokea benchi kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Nahodha, John Raphael Bocco. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa 1-0 JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 72 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 77 za mechi 33. Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya sita kati ya saba za nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, kiungo Hassan Dilunga aliyetokea benchi kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Nahodha, John Raphael Bocco. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa 1-0 JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 72 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 77 za mechi 33. Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya sita kati ya saba za nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, kiungo Hassan Dilunga aliyetokea benchi kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Nahodha, John Raphael Bocco. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MCHEZO unaoendelea kwa sasa Uwanja wa Uhuru ni kati ya wenyeji Simba wakimenyana na JKT Tanzania. Kwa sasa ni kipindi cha pili na hakuna mbabe ambaye ameona lango la mpinzani wake kwa sasa. JKT Tanzania wanafanya mashambulizi kwa kushtukiza kuliandama lango la Deogratius Munish. Mashabiki waliojitokeza hapa Uhuru sio wengi sana kutokana na leo kuwa siku ya kazi. Nahodha wa Simba John Bocco alitolewa kipindi cha kwanza nafasi yake imechukuliwa na kiungo Hasan Dilunga Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars
MAGOLI YOTE: SIMBA VS ALLIANCE SPORTS ( 2 - 0) Mtanange kati ya klabu ya Simba SC na Alliance umemalizika kwa klabu ya Simba kuifunga Alliance mabao (2-0)..... Mtanange huo umechezwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo bao la kwanza la Simba limewekwa kimiani na Kiungo wake, Haruna Niyonzima, huku bao la pili likiwekwa kimiani na Emmanuel Anord Okwi, aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Nahodha, John Bocco.... #SIMBAVsALLIANCE https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho