Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa 1-0 JKT Tanzania Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 72 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 77 za mechi 33. Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya sita kati ya saba za nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, kiungo Hassan Dilunga aliyetokea benchi kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Nahodha, John Raphael Bocco. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/kidanistars