Baada ya kuanza kuanza vibaya ligi kuu licha ya usajili wa kushtua, timu ya Singida United, ilipata ushindi wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Mbao FC ya Mwanza. Mchezo huu ulifanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwa sababu uwanja wao wa Namfua mjini Singida ulikuwa bado kwenye matengenezo
Nahodha wa timu ya Singida United inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa, Mudathir Yahya amedai wameshinda mchezo wao dhidi ya Mbao FC baaba ya kufanya marekebisho ya mchezo wao uliopita ambao walifungwa. Katika mchezo huo uliochezeka katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Singida iliondoka na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya Mboa Fc.