YANGA WALIA NA NJAMA ZA KUUMIZWA WACHEZAJI WAO CHAMAZI
Yanga SC imelipa kisasi kwa kuitandika Azam FC mabao 2-1 kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.... Yanga imepata mabao yake yote mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Pacome Zouzoua dakika 11 na Prince Dube dakika ya 34, huku Azam FC wakipata bao lao dakika ya 81. Tazama magoli....
Magoli kutoka kwa Israel Patrick Mwenda, Clement Mzize na Prince Dube yameipa Yanga ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC ukipigwa kwenye Dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Hiki ni kisasi kwa Yanga dhidi ya Tabora United, ikikumbkwa mchezo wa kwanza waliokutana msimu huu, Yanga ilipoteza nyumbani kw akichapo cha mabao 3-1 kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.
Azam FC imeitandika Singida Black Stars mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi..... Magoli ya Azam FC yametoka kwa Feisal Salum na Jhonier Blanco huku Singida wakpata bao lao kupitia kwa Elvis Rupia...
Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
Yanga SC imepoteza mchezo wa pili mfululizo kwenye ligi baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo Azam Complex, Chamazi. Offen Chikola amefunga magoli mawili dakika ya 19 na 45 ... huku Nelson Munganga akifunga la tatu dakika ya 78. Goli la kufutia machozi kwa Yanga limefungwa na Clement Mzize dakika ya 90. Yanga pia walipata penati dakika ya 45 ikipigwa na Stephane Aziz ki lakini ikadakwa na golikikpa Hussein Masalanga....
Baada ya kushinda mechi nane mfululizo, Yanga SC leo imepoteza kwa mara ya kwanza kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi. Goli pekee la mchezo limefungwa na Gibril Sillah dakika ya 33 ikiwa ni dakika 10 baada ya beki wa Yanga kutolewa kwa kadi nyekundu..... Hili hapa ni goli na kilichosababisha kadi nyekundu...
Clatous Chama amefunga goli moja na kutoa assist nne, Yanga SC ikiwanyoosha Vital'O ya Burundi kwa kichapo kizito cha magoli 6-0 katika mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika #CAFCL uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi.... Waliofunga magoli hayo ni Pacome Zouzoua kwa penati dakika ya 14, Clement Mzize dakika ya 49, Clatous Chama dakika 51, Prince Dube dakika 71, Stephane Aziz Ki dakika ya 78 na Mudathir Yahya dakika ya 86.