Beki Ibrahim Hamad Abdullah Bacca amefunga magoli mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam. Magoli mengine kwenye mchezo huo yametoka kwa Prince Dube na Clement Mzize ambaye ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao....
Hatimaye Simba imevunja mwiko wa kutopata ushindi kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Kagera Sugar, baada ya leo kuitandika magoli 5-2, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania. Magoli ya Simba yametoka kwa Shomary Kapombe 13', Jean Charles Ahoua 44', Fabrice Ngoma 53, na Stephen Desse Mukwala aliyefunga mawili dakika ya 66 na 85. Magoli ya Kagera Sugar yamefunga na Datius Peter dakika ya 79 na Cleophace Mkandala dakika ya 90. Ilikuwa ni mechi ambayo pia imemshuhudia kwa mara ya kwanza kiungo mpya wa Simba, Ellie Mpanzu aliyecheza kwa takriban dakika 70.
Tazama magoli yote matano yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC Premier League kati ya Yanga SC dhidi ya Mashujaa FC. Yanga imeshinda kwa jumla ya magoli 3-2 Magoli yote matatu ya Yanga yamefungwa na Prince Dube Magoli ya Mashujaa FC yamefungwa na Idrisa Stambuli na David Ulomi
Lionel Ateba amefunga magoli mawili na kuipa Simba ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ken Gold, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Tazama highlights....
Azam FC imekula mweleka ikipokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Tabora United mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara kwenye Dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Heritier Makambo amefunga goli la kwanza kwa tabora United na kusababisha goli la pili ambalo golikipa Mohamed Mustafa amejifunga...... Goli pekee la Azam FC limefungwa na beki Yoro Diaby.
"Wachezaji wako tayari, viongozi wako tayari" - Maneno yaliyosikika wakati Meneja wa Habari na Mawasiliano wa @yangasc, @alikamwe akifanya mahojiano na viongozi wa msafara waliombatana nao DR Congo kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe. Aidha, Kamwe ameeleza kwamba mashabiki wa Yanga tayari wapo mjini Lubumbashi kwa ajili ya kuwapa nguvu wachezaji kwenye mchezo huo wa Jumamosi Desemba 14, 2024. Game itapigwa saa 10:00 jioni na itakuwa LIVE #AzamSports1HD Mhariri ✍ @abuuyusuftz #CAFChampionsLeague #LigiYaMabingwaAfrika #CAFCL #YangaSC #TPMazembe
Yanga imerejea kwenye njia ya ushindi baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, ambapo leo imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Majaliwa Stadium, Ruangwa, Lindi. Magoli ya Yanga yametoka kwa Kennedy Musonda dakika ya 50 na Pacome Zouzoua dakika ya 68.
Yanga imerejea kwenye njia ya ushindi baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, ambapo leo imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Majaliwa Stadium, Ruangwa, Lindi. Magoli ya Yanga yametoka kwa Kennedy Musonda dakika ya 50 na Pacome Zouzoua dakika ya 68.