Azam FC imeitandika Singida Black Stars mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi..... Magoli ya Azam FC yametoka kwa Feisal Salum na Jhonier Blanco huku Singida wakpata bao lao kupitia kwa Elvis Rupia...
Tazama matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye mchezo wa NBC Premier League kati ya Pamba Jiji dhidi ya Simba SC. Simba imeshinda kwa goli 1-0 na mfungaji ni Leonel Ateba.
Yanga SC imepoteza mchezo wa pili mfululizo kwenye ligi baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa tabora United, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo Azam Complex, Chamazi. Offen Chikola amefunga magoli mawili dakika ya 19 na 45 ... huku Nelson Munganga akifunga la tatu dakika ya 78. Goli la kufutia machozi kwa Yanga limefungwa na Clement Mzize dakika ya 90. Yanga pia walipata penati dakika ya 45 ikipigwa na Stephane Aziz ki lakini ikadakwa na golikikpa Hussein Masalanga....
Simba SC imeichakaza KMC mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam..... Magoli ya Simba yamefungwa na Awesu Ally Awesu dakika ya 25, Jean Charles Ahoua mawili dakika ya 38' kwa penati na dakika ya 69', na lingine limetoka kwa Edwin Balua dakika ya 66. Haya hapa magoli yote manne.....
Baada ya kushinda mechi nane mfululizo, Yanga SC leo imepoteza kwa mara ya kwanza kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi. Goli pekee la mchezo limefungwa na Gibril Sillah dakika ya 33 ikiwa ni dakika 10 baada ya beki wa Yanga kutolewa kwa kadi nyekundu..... Hili hapa ni goli na kilichosababisha kadi nyekundu...
Steven Mukwala ameifungia Simba goli pekee na la ushindi dakika ya mwisho ya mchezo, dhidi ya Mashujaa FC, kwenye Dimba la Lake Tanganyika, Kigoma..... Tazama matukio yote muhimu ya mchezo huu.... Hii ni #NBCPremierLeague
Pacome Zouzoua amepiga goli pekee na la ushindi kwa Yanga ikiitandika Singida Black Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar.. Hii ni mechi ya ligi kuu ya NBC #NBCPremierLeague
Mwamuzi mstaafu wa soka Osman Kazi ameondoa utata wa maamuzi kwenye matukio yaliyojiri kwenye mchezo wa NBC Premier League kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC uliopigwa Oktoba 19, 2024.